Kulingana na kamishna wa polisi wa kaunti ya Migori, Seif Idd Matata na kamanda wa polisi wa Migori David Kirui polisi walipata habari kuhusu bangi hiyo kutoka kwa umma na kuelekea katika shamba hilo la ekari tatu kuanza kuing’oa.
Maafisa hao wakuu wa usalama wa kaunti ya Migori waliamrisha maafisa hao kutoa ulinzi kwa bangi hiyo na kutaka bangi hiyo kupelekwa katika afisi za kamishna wa kaunti ya Migori ambako iliteketezwa kwa kuchomwa na mafuta ya petrol.
Polisi wamedai kuwa kaunti ya Migori imekumbwa na visa vingi vya bangi kunaswa katika maeneo tofauti na kuchangia katika ukosefu wa usalama mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Wameapa kumaliza visa vya ulanguzi wa madawa ya kulevya ikiwemo bangi na aina tofauti ya mihadarati.
