Kulingana na mwanadada huyo, wawili hao walikosana wakti wa uchaguzi wakti ambapo mumewe alimueleza kuwa atasafiri hadi maeneo ya Magharibi mbali na kwao Nakuru.
"Venye nilikuja nyumbani network ya simu ilipotea na nyumbani hakuna kadi za simu kwani hatungeweza kuwasiliana na mume wangu.
Sasa baada ya wiki moja nilimpigia mume wangu lakini hakushika simu, hapo akanitumia ujumbe akiuliza mbona sikuwasiliana naye mda huo wote na hapo tukajibizana." Alijieleza akidai kuwa mumewe Eric yuko Nakuru.
Wawili hao wana mtoto mmoja wa miaka minne na wameishi pamoja kwa miaka mitano.
"Msamaha nilimpa kitambo lakini nilimuambia anipe mda kidogo nitulie. Unajua wakati mwingine inafaa uketi uanze kufikiria maisha yako kwani kila mara ni kununa tu kwa nyumba, na mwenyewe anajua." Alijieleza bwana Eric.
Pata uhondo kamili.
&feature=youtu.be