logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tob Cohen kuzikwa leo, Mjane Sarah Wairimu aomba awepo

Tob Cohen kuzikwa leo, Mjane Sarah Wairimu aomba awepo

image
na

Dakia-udaku02 October 2020 - 03:28
Sarah-Wairimu-Cohen
Mawakili wa Sarah Cohen wanafanya kila juhudi kuona kwamba amehudhuria hafla ya mazishi itakayofanyika leo.

Hafla hii ilitarajiwa kufanyika jana ila haikuwezekana kwa ukosefu wa idadi inayotosha ya makuhani.

Sarah na Bernard walikuwa wametafuta makuhani 8 kiwango kidogo cha wanaotakikana.

Soma hadithi nyingine:

Jaji wa mahakama kuu Stella Mutuku alikuwa ametoa amri kuwa mjane Sarah apelekwe na maafisa wa usalama hadi makaburi ya wayahudi saa nane leo.

Mazishi yatakuwa ya faragha sana na yatafuata mila na itikadi za dini ya wayahudi.

Murgor alitangaza jana kuwa hafla hii itakuwa leo saa nane unusu.

Soma hadithi nyingine:

“Mazishi ya Tob Cohen yameahirishwa hadi kesho (Leo) saa nane unusu. Ni makuhani 8 kati ya 10 waliopatikana na Rabbi kwa mujibu wa itikadi za wayahudi."

“Tutafuta ugeuzi wa amri hiyo ya Sarah kuwepo. Hii kwa sababu amri tuliyonayo ilikuwa ya jana."

Jaji Stella Mutuku alitoa amri hiyo baada ya wote wanaohusika kukubaliana awe katika hafla hiyo.

Naibu wa DPP alihoji kuwa haoni tatizo Sarah kushuhudia mazishi ya mmewe.

Soma hadithi nyingine:

"Itikadi za mazishi zitakwenda sawa na mila za wayahudi na zitaendeshwa na viongozi wanaohusika wa jamii hiyo” Amesema Ombeta.

Kwa mujibu wa Murgor na Cliff, DPP,DCI na viongozi wa idara ya mahakama wameombwa na Sarah na Gabrielle kuendesha hafla hiyo.

Mwili wa bilionea huyu ulipatikana wiki iliyopita Ijumaa baada ya kupotea kwa wiki 8.

Mwili huu uliokuwa umeanza kuoza ulipopatikana Ijumaa alasiri .

Ulikuwa umefungwa mara kadhaa ndani ya mifuko ya plastiki.

Cohen aliripotiwa kutoweka kutoka boma lake la Lower Kabete jijini Nairobi mnamo Julai 19 na 20.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved