Kocha mkuu wa Harambee stars Jacob “Ghost” Mulee anai imani Kenya itawalaza Comoros katika mechi ya kufuzu AFCON Jumatatno ijayo, baada ya wachezaji wake kuonyesha udhabiti mkubwa kambini. Ghost anawaongoza wachezaji ugani Kasarani, huku Ayub Timbe, Teddy Akumu na Cliff Nyakeya wakiwa wachezaji wa peke wa kulipwa waliofika kambini.
Wachezaji wengine akiwemo nahodha Victor Wanyma wanatarajiwa wikendi hii.
Mlinzi wa kimataifa wa Kenya David Cheche Ochieng amejiunga na Mathare United kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Cheche anayeondoka Al Ansar ya Saudi Arabia, hapo awali alichezea Tusker na AFC Leopards na alishinda kombe la ligi kuu na wanamvinyo. Cheche anatarajiwa kuleta uzoefu mkubwa baada ya wachezaji mashuhuri kuhama klabu hio msimu huu.
Comoros imetangaza kuwa mashabiki wataruhusiwa kutazama moja kwa moja mechi yao na Harambee stars nchini humo. Licha ya janga la corona kukita mizizi, maafisa wa kisiwa hicho wameamua mashabiki elfu 5, pekee watakubaliwa uwanjani.
Kenya itaalika Coromos katika mkondo wa kwanza wa kufuzu kwa AFCON Jumatano ijayo ugani Nyayo bila mashabiki, kabla ya mechi ya marudiano wikendi ijayo.
Kwingineko, wasmamizi wa ligi ya daraja la pili nchini Uingereza, wamethibitisha kuwa klabu ya Derby County imenunuliwa na bwenyenye wa Abu Dhabi Sheikh Khaled. Kabla ya kununua hisa kubwa zaidi katika klabu hiyo ya EFL Khaled hapo awali alijaribu kununua Liverpool na Newcastle United ila hawakufanikiwa.
Hii ina maana kuwa atawekeza katika klabu hiyo na angalau kuwapandisha katika ligi kuu Uingereza.