Si kila mmoja yuko katika uhusiano wa kimapenzi ana upendo wa kweli kwa mwenake ilhali kuna wale wamo katika uhusiano huo kwa maana wanahisi upweke na wengine wamo kwa ajili ya pesa ya mmoja wao.
Karne hii ya sasa wanawake wengi hutarajia wanaume ambao wamo katika uhusiano nao wagharamie kila kitu kama vile pesa ya saluni,kulipa kodi ya nyumba na kadhalika.
Pia kuna wale wako katika uhusiano huo kulipiza kisasi kama aliumizwa katika uhusiano wake wa kimapenzi wa awali.
Lakini husitie shaka kwa maana nitakupa ishara za mapenzi bandia ambazo unapswa kuchunguza kutoka kwa mpenzi wako;
1.Hawana wasiwasi
Hata ukipigiwa simu na mwanamke au mwanamume mwingine hana haja ya kujua haswa ni nani huyo aliyekupigia simu.
Pua ukimfania utani kuwa muachane kwa kweli utampata tu amekaa hana wasiwasi wowote wa kuuliza kwanini haswa ulichukua uamuzi huo.
2.Hawakutani nawe wala kuwa na haja ya kukutana nawe
Mkizungumza kwa simu haya basi ametosheka hana haja ya kusema kwamba anataka kukutana nawe ili muonane.
Ama mkionana kama leo ata mazliza mwezi mzima bila ya kuwa na haja ya kukutana nawe tena.
3.Ana umbali wa kihemko
Hata ukifanya nini kwa ajili ya mapenzi yenu hana mhemko wowote kwa ajili ako ilhali anasema kwamba anakupenda na moyo wake wote.
4.Wana hisia nyingi
Endapo umemkosea mwenzako haya basi kwa muda mfupi atakuwa na hisia ambazo zinachangia uhusiano wenu uishe kwa muda mrefu.
Hana heshima kwako wala unyenyekevu atakuambia chochote au lolote ili kukuudhi.
Baadhi ya watu wa kisasi hiki cha sasa hawatambui umuhimu wa mapenzi wala kutambua mapenzi ya kweli.