logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Naomba nihudumu kama rais wenu kuanzia 2022,' Gavana Kivutha Kibwana asema

"KLM ni muungano wa mashirika ya kutetea haki na wanaoleta mageuzi kwenye vyama

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku09 December 2020 - 07:57

Muhtasari


  • Kivutha KIbwana aomba kuwa rais wa jamuhuri ya kenya mwaka wa 2022
  • Kibwana alisema kuwa anatafuta uungwaji mkono na chama cha KLM

Gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana ametangaza kuwa atawania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facbook kibwana alikuwa na haya ya kusema,

"Naomba nihudumu kama rais wenu kuanzia 2022. Natafuta uungwaji mkono na Kongamano La Mageuzi ( KLM)

"KLM ni muungano wa mashirika ya kutetea haki na wanaoleta mageuzi kwenye vyama vya kisiasa. Tutaunda muungano wa kuleta ushindi." Aliandika KIbwana.

Kivutha ameungana na kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua, mwanaharakati David Ndii, Bonface Mwangi na wengine chini ya vuguvugu la Linda Katiba.

Aliingia kwenye siasa 2002 wakati ambapo alichaguliwa kama mbunge wa Makueni na kisha kuzawadiwa na aliyekuwa rais Mwai Kibaki na kiti cha uwaziri.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved