Jamii ina maoni mengi na ubaguzi juu ya mapenzi,Kama matokeo watu mara nyingi huhisi kushinikizwa kukaa katika uhusiano, hata ikiwa hawaridhiki nayo, na wanajisikia kuwa na hatia kwa kuwa hawana wapenzi.
Lakini usisahau kwamba unaweza kuwa peke yako lakini sio upweke. Kuwa katika uhusiano na wewe kweli kuna faida nyingi.
Lakini faida hizo ni kama gani, pia kuna sababu ambazo zinathibitisha kwamba kuwa 'single' inaweza kuwa bora kuliko kuwa kwenye uhusiano.
Sababu hizo ni kama vile zifuatavyo;
1.Ni vyema kujifunza kuwa mkarimu kwako kwanza
Baada ya kumpenda mpenzi wako kuna baadhi ya wale usahau kujipenda na kuwa wakarimu kwao wenyewe huku wakiwapa wenzao kipaumbele katika maisha yao.
2.Kujikuwa single
Data huonyesha kwamba watu wengi huwakashifu sana wanaume na wanake ambao hawana wapenzi, huku wasifahamu kama kuwa 'single' ni chaguo la mtu.
3.Kuwa 'single' kutakufanya huwe mwenye afya
Najua unauliza kuwa mwenye afya aje, kwa kweli kila mtu ana hisia sikatai, lakini utakuwa na afya njema kwa maana huna mtu ambaye anakupa mawazo akilini mwako.
Yaani uko huru kufanya kile wataka bila kuitisha mtu yeyote ruhusa.
4.kukimbiza mapenzi kunaweza kufanya maisha yako yawe mabaya
Tumewaona wengi wakiuana kwa ajili ya mapenzi, au mtu kuwa na msongo wa mawazo kwa ajili ya mapenzi.
Mapenzi hayalazimishwi.
5.Kuwa 'single' kutakufanya kuwa na uhusiano wa kipekee
Kuwa 'Single kutakufanya kuwa na uhusiano wenye nguvu na wa kipekee kwa maana, wakati mwingi unatumia ukiwa na marafiki na wala sio mpenzi wako.