logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je kujamiiana kunaweza kuathiri mabadiliko ya tabia nchi?

Mfuko wa Idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa unakadiria karibu kondomu bilioni 10 za mpira za kiume hutengenezwa kila mwaka na nyingi hutupwa kwenye jalala.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku27 October 2021 - 05:25

Muhtasari


•Mfuko wa Idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa unakadiria karibu kondomu bilioni 10 za mpira za kiume hutengenezwa kila mwaka na nyingi hutupwa kwenye jalala.

Ni namna gani maisha yetu ya kujamiiana yana athari katika mabadiliko ya tabia nchi?

Tunapofikiria juu ya njia mbalimbali ambazo zinaweza kupunguza matumizi yetu ya kaboni, maisha yetu ya mapenzi yanakuwa sio kipaumbele.

Bado ufuatiliaji wa kwenye tovuti kuhusu bidhaa endelevu kama vile kondomu na bidhaa za uzazi wa mpango ambazo zimekuwa zikiongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Kujamiiana ambako ni rafiki kimazingira , kukoje?

"Kwa wengine, kuwa rafiki wa mazingira katika kujamiiana kunamaanisha kutumia njia mbadala kama vile mafuta ya vilainishi, mwanasesere, mashuka na kondomu ambazo zina madhara kidogo kwenye sayari," anaelezea Dk Adenike Akinsemolu, mwanasayansi wa mazingira endelevu kutoka Nigeria.

"Kwa wengine, inahusisha kupunguza uharibifu katika kuanzishwa kwa wafanyakazi wa ngono na mazingira. Mifano yote miwili ni halali na muhimu."

Mfuko wa Idadi ya watu wa Umoja wa Mataifa unakadiria karibu kondomu bilioni 10 za mpira za kiume hutengenezwa kila mwaka na nyingi hutupwa kwenye jalala.

Hiyo ni kwa sababu kondomu nyingi zimetengenezwa kutoka kwa mpira na hutumia ladha ya viungo na kemikali, ambazo haziwezi kutumika zaidi ya mara moja.

Dr Adenike Akinsemolu ni mtaalamu wa maendeleo endelevu kutoka Nigeria

Mafuta mengi ya vilainishi yanatokana na petroli, Hii imesababisha kupanda kwa maji au bidhaa za asili. Na bidhaa za nyumbani zimepata umaarufu mkubwa sana.

Dk Tessa Commers ana wafuasi zaidi ya milioni moja wanaotazama video zake za TikTok kuhusu afya ya ngono. Video yake iliyotazamwa zaidi - ambapo karibu watu milioni nane wameangalia - inaonesha namna mafuta ya vichocheo yanayotengenezwa nyumbani yaliyotengenezwa na wanga na maji.

"Vilainishi vinavyotengenezwa na maji, kondomu ambazo hazina kemikali na zimetengenezwa na vitu vya asili ni chaguo zuri kwa kujifurahisha na kukumbatia maisha endelevu ya ngono," anasema Dk Akinsemolu. "Sio tu kwamba husababisha uharibifu mdogo kwa mazingira lakini huwapa watumiaji wao wakati mzuri."

Hata hivyo, tahadhari lazima ichukuliwe katika baadhi ya bidhaa za kijani kibichi, kwani zingine haziwezi kutumiwa na kondomu nyingi kwa sababu zinaweza kusababisha kupasuka. Na kabla ya kufanya maamuzi yoyote kuhusu uzazi wa mpango, unashauriwa kuzungumza na daktari au mtaalamu wa kupanga uzazi.

Wanasesere wanaotumika kwaajili ya kujamiana ni bidhaa nyingine ambayo inaongeza katika matumizi ya plastiki , ingawa kuna mbadala wa kununua vifaa vinavyotumika baada ya matumizi (rechargeable )pia husaidia kupunguza taka. Kuna hata wanasesere wa ngono wanaotumia nishati ya jua.

Kampuni kama vile LoveHoney pia hutoa msaada wa wanasesere wa ngono ambao husaidia katika kuchakata wanasesere wa zamani.

Ni sehemu gani nyingine inaweza kupunguza taka?

Vilevile kuna sehemu zisizo wazi za maisha yetu ya kujamiiana ambapo mabadiliko yanaweza kufanywa ili kupunguza taka.

Kununua nguo za ndani na nguo zilizotengenezwa kwa maadili, kuepuka kufanya ngono wakati wa kuoga, kupunguza kutumia maji ya moto , kutowasha taa na kuchagua nguo zinazoweza kutumika tena zikifuliwa ni njia za kupunguza athari za taka kwenye sayari.

Kama vitu vingi tunavyonunua, ufungashaji mara nyingi husababisha matumzi ya taka. Lauren Singer, mjasiriamali na mshawishi wa kutotumia taka kutoka New York, anasema hapa ndipo kampuni nyingi zinaweza kuleta mabadiliko.

Kondomu, mafuta ya vilainishi na dawa za kuzuia mimba za kila siku ni bidhaa zinazoweza kuzalisha vifungashio ambavyo huishia kwenye jalala. IUDs (vifaa vya vipandikizi) kama ni njia za uzazi wa mpango za muda mrefu, ambazo zina taka kidogo lakini huja na hatari zake.

Lauren anaishi karibu bila taka na, tangu 2012, amekusanya chochote ambacho hakihitaji kwenye kopo.

Hauwezi ukapata kondomu kwenye mtungi wa Lauren na, kwa kuwa ndizo njia pekee za kuzuia mimba zinazofaa dhidi ya magonjwa ya zinaa, anawataka wapenzi wake wote kupima kabla ya kujamiiana nao.

"Nina mpenzi mwenye mke mmoja sasa, lakini ikiwa hujisikii vizuri kumwomba mpenzi wako kupima kabla ya kujamiiana naye, basi labda hupaswi kujamiiana naye kabisa," Lauren anasema.

Hata hivyo, anasema hakuna kitu kisichoweza kudumu kama mimba isiyotakiwa au ugonjwa wa zinaa.

"Tunapaswa kuzingatia ni taka gani inafaa kuzalisha na zipi hazifai," anasema. "Watu hawapaswi kutumia kondomu au kuchukua udhibiti wa kuzaliana kwa sababu ya kipengele cha taka - ni muhimu zaidi kukulinda wewe na mpenzi wako."

Dk Akinsemolu anakubali. "Ngono salama, iwe kwa kutumia bidhaa rafiki kwa mazingira au la, ndiyo endelevu zaidi kwa watu na sayari kwa muda mrefu," anasema.

Athari ya hali ya hewa ya kuzaliana

Athari ambayo inatuleta katika hatua nyingine ambapo ngono na mazingira hugongana -katika kupata watoto.

Kulingana na utafiti wa mwaka 2017, kuishi bila gari huokoa takriban tani 2.3 za CO2 kwa mwaka, wakati kushikamana na lishe inayotokana na mimea huokoa tani 0.8. Kwa kulinganisha - ikiwa unaishi katika ulimwengu ulioendelea - kutokuwa na mtoto kunaokoa takriban tani 58.6 kwa mwaka.

Kiwango cha kaboni katika nchi ambazo hazijaendelea ni cha chini sana, huku mtoto wa nchini Malawi akikadiriwa kuwa si zaidi ya tani 0.1.

Alexandria Ocasio-Cortez katika mkutano wa C40 huko Copenhagen mwaka 2019

Baadhi ya watu mashuhuri wamejadili kutoridhishwa kwao kuhusu kupata watoto.

Prince Harry aliliambia jarida la Vogue mnamo 2019 kwamba yeye na Duchess wa Sussex watakuwa na watoto wawili, akitoa mfano wa mazingira kama sababu kuu katika uamuzi huu.

Vile vile, mbunge wa Marekani Alexandria Ocasio-Cortez alisema kwenye Mkutano wa Mameya wa Dunia wa C40 mwaka 2019 kwamba alikuwa "mwanamke ambaye ndoto zake za kuwa mama sasa zina ladha chungu kwa sababu ya kile ninachojua kuhusu siku zijazo za watoto wetu".

Viwango vya kuzaliwa vimepungua katika nchi nyingi ulimwenguni. Mwenendo wa miongo kadhaa kwa hakika hauwezi kuelekezwa kwa mabadiliko ya hali ya hewa pekee.

Lakini uchunguzi wa kimataifa wa wanasayansi wa Uingereza mwaka huu ulipata robo tatu ya vijana 10,000 waliohojiwa walikubali "baadaye ilikuwa ya kutisha". Baadhi ya 41% ya waliohojiwa "walisitasita kupata watoto" wakitaja sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Maelezo ya video,

Afisa usalama barabarani wa Iraq anayeongoza magari katika kiwango cha nyuzijoto 50

Sina watoto

Tanmay Shinde anaishi Mumbai, India, na ameamua kuwa hatazaa watoto kwa ajili ya kutunza mazingira. IPCC imetabiri kuwa mji wake unaweza kuzamishwa na kuongezeka kwa kina cha bahari ifikapo mwaka 2050.

Familia yake imeona uamuzi wake kuwa mgumu kueleweka, ingawa anakubali kama mwanaume anaweza kuwa na mapendeleo zaidi kuliko mwanamke nchini India karibu kwa kuwa na imani hii.

"Familia nchini India ni za kitamaduni na zina utamaduni wa kufuata mila na desturi za zamani," anasema. "Kupata watoto ni moja ya mambo muhimu zaidi katika maisha baada ya ndoa na kuna shinikizo kubwa kutoka katika kijamii kuendeleza utamaduni huu.

Tanmay Shinde hataki kupata watoto ili kulinda mazingira, labda tu viongozi wa dunia wakifanya maamuzi makubwa ya kulinda dunia

Je, ataweza kubadili mawazo yake?

"Sayari salama na mtindo wa maisha endelevu ni sharti la kuwa na watoto kwa hivyo, isipokuwa kama kuna maamuzi madhubuti yaliyofanywa na mabadiliko makubwa ya kupunguza uzalishaji wa kaboni na kukomesha ongezeko la joto duniani, sidhani kama nitapata watoto."

Profesa Kimberly Nicholas, profesa mshiriki katika Chuo Kikuu cha Lund, nchini Sweeden, aliandika pamoja utafiti ambao ulisema watoto katika ulimwengu ulioendelea wana athari mbaya sana juu ya utoaji wa kaboni.

Hata hivyo, habishani kuwa watu wasizae watoto.

"Sio jukumu langu kuidhinisha au kutilia shaka chaguzi za kibinafsi za watu," anasema. "Ni haki ya binadamu kuamua kwa uhuru ikiwa wanataka kupata mtoto. Ninachofanyia kazi ni ulimwengu ambapo watoto ambao tayari wako hai wana sayari salama na jamii."

Badala yake anapendekeza watu watumie muda mwingi kufikiria upya tabia zao za kusafiri "badala ya kuhangaika juu ya vifuniko na kuondoa kila kipande cha mwisho cha taka kutoka kwa uzazi wa mpango".

"Tunapaswa kuelekeza juhudi zetu pale inapoleta mabadiliko," anasema.

Profesa Kimberly Nicholas

Kama mtu ambaye ametumia theluthi moja ya maisha yake kuishi bila taka, Lauren hajaamua juu ya suala la watoto.

"Nimefikiria juu ya kuasili, ambapo nadhani ni kitu ambacho kingekuwa kizuri, lakini basi mchakato halisi wa kupata mtoto - sina uhakika," anasema.

Kama maamuzi mengine kuhusu uendelevu, anajiuliza ikiwa kupata mtoto kunaweza kuwa "chanya kabisa".

"Je, kutakuwa na faida kwa sayari kwa ujumla? Je, ninaweza kutoa thamani kwa mtoto huyu ambaye ataishi muda mrefu kuliko mimi na kuendelea kujaribu kuunda ulimwengu bora?"


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved