Wabunge wameidhinisha uteuzi wa Antony Mwaniki kuwa mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).
Nafasi hiyo iliachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti Stephen Kirogo baada ya kuugua mwezi Aprili
Kirogo alikuwa akihidhinishwa na kamati ya Leba na Jamii inayoongozwa na Mbunge wa Mwea, Josphat Kabinga.
Bunge linatarajiwa kujadili ripoti ya kamati baadaye siku ya jumanne 21 ili kuunga mkono au kukataa uamuzi huo. Ikipitishwa majina hayo yatapelekwa kwa Rais kwa uteuzi rasmi.
Mabadiliko haya yamefanyika baada ya bunge kufanya makao maalum ambayo ya nia yake nikuzungumzia miswada inayohusiana na uchaguzi mkuu ujao 2022 pamoja na kuidhinishwa kwa uteuzi wa PSC.
Naibu wa Spika Moses Cheboi ndiye aliendesha shughuli hio muhimu ambapo alitangaza sababu za Spika kukosa kuhudhuria kikao hicho cha wabunge
"Alipata ajali ndogo ofisini alipokuwa akijaribu kuvuta droo. Kiti chake kiliteleza na aliumia mkono wake wa kulia, bega na mgongo"Cheboi aliwatangazia wanachama kuwa spika alifanyiwa upasuaji mdogo na akashauriwa kupata nafuu nyumbani.