logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Alikuwa nataka akumbukwe milele,'Rappa Habib afichua anachopeza zaidi kuhusu kaka yake E-Sir

Habib anasema zamani  aliathiriwa na watu kumfananisha na Esir lakini hilo sasa ni historia.

image
na Radio Jambo

Burudani20 January 2022 - 10:22

Muhtasari


  • Rappa Habib afichua anachopeza zaidi kuhusu kaka yake E-Sir
  • Habib anasema zamani  aliathiriwa na watu kumfananisha na Esir lakini hilo sasa ni historia

Rapper, Habib Wangui amefunguka kuhusu kile anachokipeza zaidi kuhusu marehemu kaka yake Issah Mmari almaarufu E-Sir.

E-Sir alifariki miaka 18 iliyopita baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani alipokuwa akitoka kwenye shoo.

Katika mahojiano maalum na Mpasho, Habib sasa anasema anachokosa zaidi ni jinsi marehemu kaka yake alivyokuwa akifanya kazi kwa bidii.

"Nilifurahi niliposikia wazo la kushiriki katika 'Bandana Ya Esir kwa sababu nakumbuka Esir aliniambia sababu ya kufanya muziki ni ili akumbukwe milele."

Kwa hivyo nilikuwa kwenye wazo la kufanya hayo.

"Nakumbuka jinsi yeye (Esir) alivyokuwa akifanya kazi kwa bidii. Kuna wakati alikuwa akisafiri kutoka nyumbani hadi zilipo studio."

Habib anasema zamani  aliathiriwa na watu kumfananisha na Esir lakini hilo sasa ni historia.

"Hapo zamani iliniathiri lakini sio tena,Nimejikubali jinsi nilivyo, mwisho wa siku mimi ni Habib sijawahi kujiona mtu mashuhuri."

Alipoulizwa kuhusu kile anachokosa zaidi kuhusu Esir, Nameless alijibu akisema anapenda jinsi rapper huyo alivyokuwa mcheshi.

'Mambo matatu yalionekana wazi, Alikuwa mchapakazi, mwenye nidhamu na mnyenyekevu sana."

Alikuwa na talanta ya hali ya juu, mpenda furaha."

Habib ni miongoni mwa wasanii ambao hivi majuzi walishiriki katika wimbo 'Bandana Ya Esir wimbo uliotayarishwa kama kumbukumbu kwa marehemu rapper.

Esir alijulikana zaidi kwa nyimbo kali kama vile Boomba Train, Mos Mos miongoni mwa zingine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved