Katika video moja ambayo imeteka anga za mitandao ya kijamii, wateja wa benki moja wanaonekana kuchoka kutozwa gharama za juu za huduma ya arafa na kuamua kuchukua sheria mabegani kama si mikononi.
Wateja hao wenye ghadhabu ya kupigiwa mfano wanaonekana wakiandamana na kujitoma ndani ya majengo ya benki hiyo huku walilalama mbele ya wahudumu wa benki ambao wanabaki hoi bin taabani, wasijue la kufanya ili kutuliza jazba za wateja waandmanaji.
Video hiyo ambayo ilipakiwa na mwanablogu mmoja kutoka Nigeria anayejiita Instablog9ja kwenye mtandao wa Instagram, wateja hao ilibidi wamefungiwa ndani ya benki hiyo huku njia mbadala za kuyatatua malalamishi yao zilitafutwa.
Wananchi wa taifa hilo baada ya kuona video hiyo, walimiminika kwenye sehemu ya kutoa maoni ambap wengi walitoa ushuhuda wao kwamba benki hiyo imekuwa na mazoea ya kutoza viwango vya juu vya huduma za SMS kwa wateja wao.
Baadhi ya wateja hao waliamua kulishusha timbwiri kwa vita huku wahudumu wa benki hiyo wakijitetea kwamba hakuna njia yoyote ya kuzirejesha pesa za wateja hao zilizodaiwa kupotelea katika tozo za juu za ada ya SMS.