Kuna visa, mikasa, vioja na matukio ambao huokea mpaka wakati mwingine mtu utadhani si binadamu anakitekeleza bali shetani mwenyewe katika ngozi ya ubinadamu.
Ni kisa cha kusikitisha na ambacho kimegonga vichwa vya habari katika ukanda wa Afrika mashariki baada ya mwanaume mmoja kudaiwa kumbaka mwanamke mjamzito hadi kufa.
Mwanaume huyo kwa jina Mohamed Mwanjali ambaye ni mkaazi katika mkoa wa Iringa nchini Tanzania anashikiliwa na polisi nchini humo baada ya kudaiwa kuvizia familia moja usiku na kumbaka mwanamke aliyekuwa mjamzito hadi kusababisha kifo chake.
Kulingana na taarifa zilizochapishwa na mwanahabari maarufu Millard Ayo, Mwanjali alivizia nyumbani kwa mwanamke huyo usiku baada ya mumewe kutoka kuenda kutazama pambano ya ngumi baina ya mabondia ya Tanzania waliokuwa wakimenyana wikendi iliyopita.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni, Yassin Kisogole alinukuliwa na taarifa hiyo ya Ayo akisema Mwanamke marehemu alitendewa ukatili huo usiku wa kuamkia September 25,2022 wakati Mumewe akiwa Mtaa wa jirani alipokwenda kushuhudia pambano la ndondi la Mandonga vs Abeid na kisha lile la mwisho usiku huo lililowakutanisha mabondia Twaha Kiduku vs Abdo kupitia.
Mapambano hayo yalikuwa yanapeperushwa moja kwa moja kwenye runinga.
Mume wa marehemu aliporudi nyumbani baada ya kumalizikqa kwa mapambano hayo ya ngumi, alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi wakati akiingia ndani alimuona Mtuhumiwa akitoka katika moja ya chumba na kukimbia ndipo alipojaribu kumkimbiza bila mafanikio.
Alipoingia ndani alimkuta Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimmsimulia kuwa kulikuwepo na mtu aliyevizia nyumbani humo na kumziba mama yake mdomo kabla ya kumuangusha chini na kumtendea kitendo hicho cha unyama.
Baada ya taarifa hizo Mume huyo wa Marehemu alienda kutoa taarifa Polisi, ambapo Mtuhumiwa alikamatwa na Polisi nyumbani kwake ambako alikutwa na baadhi ya vitu vya Marehemu ikiwamo simu ya mkononi na nguo ambazo alizichukua mara baada ya kutekeleza tukio hilo.