logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Moya David afungua tawi jipya la saluni ya kifahari Kitengela

Tuko wazi na tuko tayari kukuhudumia - Moya David.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku11 February 2023 - 08:10

Muhtasari


• Asante kwa mashabiki wangu wote ambao walikua familia na kwa kuwa sehemu ya safari na ukuaji pia - Moya.

Moya David

Mcheza densi David Moya amefungua tawi lingine la kinyozi chake cha kifahari katika eneo lla Kitengela kaunti ya Kkajiado miezi michache baada ya kufungua tawi la kwanza mtaani Kilimani jijini Nairobi.

Moya alidhibitisha bahari hizo kwa picha maridadi akiwa na baadhi ya vijana aliowapa kazi katika kinyozi hicho chake na kumshukuru Mungu kwa kumfungulia Baraka na uwezo wa kuweza kuwapa vijana wenzake kazi.

“Nawasilisha kwako mtoto wangu mpya Moya city Barbers tawi la Kitengela🔥maeneo ni ndani ya Kilabu ya Quiver Kitengela. Tuko wazi na tuko tayari kukuhudumia   Asante kwa mashabiki wangu wote ambao walikua familia na kwa kuwa sehemu ya safari na ukuaji pia,” Moya alisema.

Katika ufunguzi wa tawi la kwanza mtaani Kilimani, watu wengi mashuhuri walihudhuria kumpa shavu na alizungumza kutoka moyoni kuwashukuru wote waliomwaminia na kumkweza.

“Nimekuwa nikipanga hili kwa muda mrefu, nilikuwa nikiweka akiba hapo awali na niliongeza kile nimekuwa nikihifadhi sasa. Baadhi ya marafiki zangu wazuri wamekuwa wakinipa mawazo na kunishauri sana jinsi ya kutumia pesa zangu na nimekuwa nikifuatilia ushauri wao,” alisema kipindi hicho.

Mcheza densi huyo mwenye umaarufu mkubwa Tiktok amekuwa akifanya kazi yake kwa bidi kubwa na adabu iliyotukuka pindi anapopewa kandarasi ya kuwashtukizia watu kwa zawadi mbalimbali.

Mpaka sasa, David ana wafuasi Zaidi ya milioni moja kwenye mtandao wa Tiktok wakimfuatilia tu jinsi anaendesha shughuli zake za kucheza densi kwa watu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved