logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo Ijumaa

KPLC imesema mpango wa kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa ni kutokana na matengenezo ya mtandao.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku17 May 2024 - 04:26

Muhtasari


•KPLC ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

•KPLC imesema kuwa mpango wa kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa ni kutokana na matengenezo ya mtandao.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Mei 17.

Katika taarifa ya siku ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kisii na Murang'a.

Katika kaunti ya Kisii, baadhi ya sehemu za eneo la Ogembo zikiwemo Ogembo Sports Club, MRF Tyres, Junior Farms Ogembo, Getare Pri, Gituno TBC na viunga vyake zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Maporomoko na Ngoingwa katika kaunti ya Murang'a pia zitakosa huduma za umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

KPLC imesema kuwa mpango wa kukatizwa kwa umeme katika maeneo yaliyotajwa ni kutokana na matengenezo ya mtandao yatakayokuwa yakifanyika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved