Mtangazaji maarufu wa TV Betty Mutei Kyallo ameendelea kumminia mahaba tele mpenzi wake Charlie Jones huku uhusiano wao ukionekana kuchanua.
Siku ya Jumatano, mama huyo wa mtoto mmoja wa kike alitoa maoni yake chini ya chapisho la Instagram lililozungumza kuhusu wanawake kuwathamini waume zao, ambapo alisifu jukumu la kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 katika maisha yake.
Chapisho ambalo Betty alitoa maoni chini yake lilikuwa kuhusu wanawake kuwatia moyo waume zao wanapopambana na changamoto za maisha.
"Mume mpendwa, tutapitia haya. Hofu, maumivu na hali ya mkazo hivi karibuni. Nataka ujue kuwa unathaminiwa na kupendwa,” chapisho hilo lilisomeka.
Katika maoni yake, mwanahabari huyo mwenye umri wa miaka 35 alimhakikishia mpenzi wake kuhusu shukrani zake na upendo mkubwa alionao kwake.
Betty aliendelea kumsifu kijana huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa mambo ambayo amemfanyia na kumwomba Mungu aendelee kumbariki.
“@charliemny mpenzi wangu. Ninakupenda sana na ninakuthamini na jinsi ulivyosimama nami katika yote. Unanijali, unanispoil vibaya, unacheza nami kama watoto wadogo, unanienzi na unatutunza sote,” Betty alisema.
Aliongeza “Nakupenda. Mungu akubariki sana.” Uhusiano wa Betty na Charlie hatimaye ulikuja kujulikana wazi miezi michache iliyopita baada ya mtangazaji huyo wa TV kujaribu kumficha mpenzi wake kwa muda.
Hatimaye Betty Kyallo alifichua sura ya mpenzi wake mwezi Juni huku akimsifia katika ujumbe mzuri wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa.
Ufichuzi huo ulikuja saa chache baada ya mwanahabari huyu kuwajibu wakosoaji wake kwa tamko la uhakika la furaha yake, akisema kwamba yeye ni "mke mwenye furaha anayefurahia maisha ya furaha."
Betty na mpenzi wake walitumia siku ya kimapenzi huko Ngong Hills, ambapo alishiriki sala maalum na kumtakia tamu alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
"Heri ya kuzaliwa, mpenzi. Vicheko zaidi, kukumbatiana zaidi, watoto zaidi, sisi zaidi. Hii ndio. Naomba mtu wangu ashinde kila wakati. Amekuwa akishinda, lakini nataka ashinde mengi zaidi.Kwa Mungu, mke mwenye furaha, maisha ya furaha. Type shii,” aliandika.
Wawili hao hata hivyo wamekabiliwa na ukosoaji mwingi mtandaoni kuhusu tofauti zao za umri huku Betty Kyallo akiwa na umri wa miaka kadhaa kuliko mpenzi wake.