logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanahabari Kimani Mbugua afichua chanzo cha matatizo ya kiakili yaliyompelekea kupelekwa rehab

Kimani ambaye kwa miezi kadhaa iliyopita amekuwa akipokea matibabu alifichua kuwa matatizo yake yalianza kazini.

image
na Samuel Mainajournalist

Dakia-udaku29 October 2024 - 11:27

Muhtasari


  • Kimani Mbugua amefunguka kuhusu matatizo ya kiakili ambayo amekuwa akipambana nayo katika miaka michache iliyopita.
  •  Alizungumzia changamoto mbalimbali alizokutana nazo kazini ikiwa ni pamoja na shinikizo na mazingira magumu ya kazi.

Aliyekuwa mtangazaji wa TV Kimani Mbugua amefunguka kuhusu matatizo ya kiakili ambayo amekuwa akipambana nayo katika miaka michache iliyopita.

Katika mahojiano na DW, Kimani ambaye kwa miezi kadhaa iliyopita amekuwa akipokea matibabu katika Kituo cha Urekebishaji cha Wanawake cha Mombasa, alifichua kuwa matatizo yake yalianza kazini.

Mwanahabari huyo kijana alizungumzia changamoto mbalimbali alizokutana nazo kazini ikiwa ni pamoja na shinikizo na mazingira magumu ya kazi yaliyompelekea hadi kwenye hali ambayo amekuwa akihangaika kukabiliana nalo.

“Unapata umepatiwa kazi nyingi sana mpaka unashindwa kuwa na wakati wako wa kutulia na kulala vizuri,” Kimani alisema.

Aliongeza, “Ilifika mahali nikawa na kitu kinaitwa burnout.  Ukiwa na burnout, unashindwa kuendelea na kazi vizuri, kuanza kuwa na mikwaruzano pale kazini, unapata watu wanaanza kuchukiana, watu wanaanza kushindana kwa sababu hakuna mtu anajua nani ataweza kufutwa kazi leo ama kesho.”

Mwanahabari huyo wa zamani wa runinga ya Citizen hata hivyo  ameweka wazi kuwa sasa anaimarika baada ya kuhamishwa hadi kituo cha kurekebisha tabia cha Mombasa.

Kimani alihamishwa kutoka hospitali ya Mathare hadi Mombasa mnamo mwezi Mei kufuatia kuingilia kati kwa gavana wa zamani wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko.

Wakati huo, Sonko aliweka wazi kwamba alikusudia kumpeleka mwanahabari huyo katika kituo cha marekebisho ya tabia cha Hospitali ya Wanawake ya Mombasa akisema kuwa mabadiliko ya mazingira yangemsaidia katika mchakato wa kupona.

 "Kimani mbugua tayari ametoa mengi kwa ulimwengu kupitia kazi yake, na ni wakati wetu wa kurudisha matumaini, upendo na utunzaji. Tulivutiwa sana na huduma za uongozi mzima wa hospitali hiyo, ni hospitali nzuri sana yenye wahudumu wa afya waliohitimu na kitaaluma.  Kwa hiyo hata kama tutawahamishia Mombasa itakuwa tu kwa malengo ya kubadilisha mazingira ambayo yanaweza pia kuchangia pakubwa kupona kwa mgonjwa na ndiyo maana niliamua pamoja na familia kuwahamishia Mombasa Women Rehabilitation Center ambapo Conjestina Achieng yuko tuone kama watachange for good,” alisema.

Mwanasiasa huyo alikariri kuwasapoti Kimani na mwanahabari mwingine aliyekabiliwa na matatizo ya kiakili ,Eunice Omollo, katika safari yao ya kupona na kuwatakia afueni ya haraka.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved