Idara ya polisi katika taifa la Georgia imewataka wanandoa wanafanya tendo la kujamiana kufanya hivo katika vyumba vya kukodi kwa muda au kujuzuia hadi watakapofika nyumbani kwao.
Taarifa hii inajiri baada ya bwana mmoja na mpenzi wake kufanya
kitendo hicho kwenye nyazi mahali peupe kando ya barabara.
Ushauri huo wa polisi wa Lavonia nchini Georgia ulijiri baada ya
wananchi kulalalmikia tukio hilo kufanyika karibu na sehemu ya biashara kwenye barabara ya Interstate 85.
Kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Facebook Idara ya polisi ya
Lavonia mnamo tarehe 22 Oktoba, iliwaonya wapenzi wanaotumia njia ya kutoka
barabara kuu ya Interstate ya Exit 1-85 kukodi chumba au kufanya kitendo hicho
wakifika nyumbani kwao.
“Mkiamua kujamiana na mpenzi wako mkiwa barabarani, tafadhali
msijamiane kwenye nyasi kati ya McDonald’s na Raceway. Ndio, ilifanyika mchana
peupe.” Taarifa ya polisi
ilisoma kwenye Facebook.
Idara hiyo iliwaonya wasafiri wanaozuru jiji la Lavonia
dhidi ya kutekeleza uovu huo ikisema kuwa ujinga wa baadhi ya watu haujaacha
kuwashangaza.
Polisi wa Lavonia wamewashauri wapenzi kukodisha chumba kwa
ajili ya shughuli hiyo ikiwa wanahisi kufanya hivyo badala ya kufanya tabiahiyo
peupe kwenye nyasi.
“Msijamiane mchana kwenye nyasi kando ya barabara. Kama wewe ni mjinga
wa kutosha kufanya hivi, basi usisimame Lavonia. Vipi kuhusu kutumia akili.”
Idara ya polisi ya Lavonia ilishauri.
Hata hivyo, wapenzi waliokamatwa wakijamiana kando ya barabara
mchana peupe walikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kukosa maadili katika
umma.