Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya amezidi kuelezea namna anapendwa kila mahali anakokwenda wa watoto wa kike.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram, kiongozi huyo amechapisha picha inayomuonyesha akiwa na mwanamke ambaye hajamtaja jina akisema kuwa licha ya kukataa kuunga mkono sera za aliyekuwa kinara wa ODM Raila Odinga, bado watoto wa kike kutoka jamii ya Raila Odinga bado wanampenda.
Salasya amesema kuwa alipatana na msichana huyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kisumu asubuhi ya Jumatano.
“Huyu mtoto mjaluo ananipenda sana, asubuhi hii tulikutana katika uwanja wa ndege wa Kisumu. Ata kama nimekataa stori za Raila watoto wajaluo bado wananipenda na nitazidi kuwakunywa.” Aliandika Peter Salasya kwenye akaunti yake Instagram.
Salasya aidha, amesikitika kuwa alikosa kunakili namba ya msichana huyo ila pia alimtakia kila la heri akimwambia kuwa kesho yake ina mwanga kutoka kwa baraka alizompa.
“Nimekubariki ata kama sikuchukuwa nambari yako ya simu ulinifurahisha sana. Nilipenda jinsi ulisimama kwenye picha.” Alisema Salasya.
Mbunge huyo amekuwa mwenye utata katika maswala ya mapenzi hivi maajuzi akisema kuwa alikuwa na malengo ya kuoa akiwa na umri wa miaka 26 lakini bado hajapata mchumba akisema kwamba wakati wa Mungu bado haujatimia.
Vile vile, alitikisa mitandao ya kijamii haswa Instagram kwa malumbano baina yake na mwanashoshalaiti Huddah Monroe baada ya harakati ya kumchumbia mwanadada huyo kugonga mwamba.