logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Namtakia Simba kila la kheri!" Zuchu asema huku akitangaza kuachana na Diamond baada ya kuchumbiana miaka 3

Binti huyo wa malkia wa Taarab, Khadija Kopa alisema kuwa uamuzi wa kutengana ulikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

image
na Samuel Maina

Dakia-udaku13 November 2024 - 07:40

Muhtasari


  • Zuchu mnamo Jumanne alitangaza mwisho wa mahusiano yake wa miaka mitatu na bosi wake Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz.
  • Aidha, alidokeza kuwa sasa atazingatia uponyaji na kazi yake.


Malkia wa Bongo Zuhura Othman mnamo Jumanne alitangaza mwisho wa mahusiano yake wa miaka mitatu na bosi wake Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Instagram, binti huyo wa malkia wa Taarab, Khadija Kopa alisema kuwa uamuzi wa kutengana ulikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Zuchu aliendelea kufafanua kuwa tayari walikuwa wamefanyia kazi pamoja mradi ambao haujatolewa, na akabainisha kwamba kutengana kwao hakutauathiri.

"Halo watu wangu wazuri. Baada ya miaka mitatu ya kuchumbiana, mimi na Nasib tumeamua kwa dhati kuachana," Zuchu alitangaza.

Aliongeza, "Huu ulikuwa uamuzi wa pande zote mbili, tuna mradi ujao kwa hivyo usishangae utakapotolewa."

Zaidi ya hayo, mwimbaji huyo mrembo mwenye sauti ya kusisimua alimtakia kila la heri Diamond ambaye pia ni bosi wake wa WCB katika shughuli zake zijazo.

Aidha, alidokeza kuwa sasa atazingatia uponyaji na kazi yake.

"Ninawaomba watu wangu wema kuwa na sapoti yenu isioisha kwani lengo langu kuu sasa ni uponyaji na kazi yangu. Wako mwaminifu, Zuchu," alisema.

Mastaa hao wawili wa bongofleva wamekuwa wakichumbiana waziwazi na kuonyesha mapenzi yao kwa takribani miaka mitatu iliyopita. Wamesafiri pamoja, wakapeana zawadi za bei ghali, wakabusiana hadharani, na kuoneshana mapenzi mengine.

Mwishoni mwa mwezi Aprili, Zuchu alikuwa ameripotiwa kuvunja uhusiano wao wa muda mrefu huku tetesi nyingi zikizunguka hali hiyo.

 Katika taarifa yake, binti huyo wa malkia wa taarab Khadija Kopa alieleza kuwa Diamond alikuwa amemfanya ashambuliwe kwa urahisi kupitia maisha yake yenye utata.

 Alimshutumu mpenzi huyo wake kwa kumweka kwenye hatari ya kutoheshimiwa na watu, jambo ambalo sasa amechoka nalo.

 “I know mimi ni maarufu na kuongelewa ni kawaida. But kindly msipitilze kunipa sifa za uongo mradi kumpamba boss haswa kwa media ya nyumbani ambayo mnaweza pia kupata ukweli wa mambo mkasawazisha stori zenu,” Zuchu alilalamika kwenye ukurasa wake wa Instagram. 

 Aliendelea, “Hii ndio sababu hasa kwa nini niliondoka, unachoka kuwa na mwanaume anayekusukuma kwa watu utukanwe na yeye ndo anayetumika kwenye kudhalilika kwako. Mwanamke wake ndo kanyagio la kila aliyemzunguka , akiamua tu basi yeye huungana nao na kuwapa vichwa vya kunivunjishia heshima ilhali umekaa kimya na unachofanya tu ni kukaa na kumeza. Ninajaribu kuwa mtu mzuri na kiungo dhaifu katika maisha yangu ni yeye."

 Wakati huo, mwimbaji huyo mrembo alitoa wito kwa watu kuwa rahisi kwake na kumruhusu kuwa na amani.

 Alilalamika kwamba kila jambo linapotokea linalohusisha watu katika maisha ya Diamond wakiwemo wazazi wenzake na wapenzi wake wa zamani, kila mara lengo linaelekezwa kwake.

 “Hamkai kusema sababu yeye, anayesababisha mtu unataka kuondoka zake. Baby mama wakiamka na hasira waje na wao wanakutupia attitude zao kwa Zuchu. Maex nisiowajua content yao wanapewa wakusema ni Zuchu. Maadui zangu ashirikiane nao wakikaa na huyo mwanaume anawapa nguvu ni Zuchu,” aliandika.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved