logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond na Zuchu wanarudiana wiki chache baada ya kutengana

Wawili hao walionekana wakiburudika pamoja na kusherehekea katika hafla iliyokusudiwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Zuchu.

image
na Samuel Maina

Dakia-udaku25 November 2024 - 07:39

Muhtasari


  • Mapema mwezi huu, Zuchu alitoa taarifa na kutangaza kuwa amemaliza uhusiano wake wa miaka mitatu na bosi wake Diamond Platnumz.
  • Matukio ya Jumapili, hata hivyo, yanaonekana kuthibitisha kuwa mambo ni sawa kati ya mastaa hao wawili na wamefufua mapenzi yao.


Mastaa wa Bongo Diamond Platnumz na Zuhura Othman almaarufu Zuchu wanaonekana kurudiana tayari wiki mbili tu baada ya kuripotiwa kutengana.

Mapema mwezi huu, Zuchu alitoa taarifa na kutangaza kuwa amemaliza uhusiano wake wa miaka mitatu na bosi wake Diamond Platnumz.

Siku ya Jumapili jioni hata hivyo, wawili hao walionekana wakiburudika pamoja na kusherehekea katika hafla ambayo ilikusudiwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Zuchu.

Mastaa hao wawili wa bongo fleva walionekana wakicheza pamoja, wakiimba pamoja na hata kuburudika pamoja kwenye hafla hiyo iliyofanyika nchini Tanzania.

Zuchu aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 31 mnamo Novemba 22, lakini Diamond hakumsherehekea hadharani kama katika siku za nyuma. Hii ilionekana kuthibitisha kwamba wawili hao walikuwa wametengana.

Matukio ya Jumapili, hata hivyo, yanaonekana kuthibitisha kuwa mambo ni sawa kati ya mastaa hao wawili na wamefufua mapenzi yao.

Mapema mwezi huu, Zuchu alitangaza mwisho wa mahusiano yake wa miaka mitatu na bosi wake Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa Instagram, binti huyo wa malkia wa Taarab, Khadija Kopa alisema kuwa uamuzi wa kutengana ulikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili.

Zuchu aliendelea kufafanua kuwa tayari walikuwa wamefanyia kazi pamoja mradi ambao haujatolewa, na akabainisha kwamba kutengana kwao hakutauathiri.

 "Halo watu wangu wazuri. Baada ya miaka mitatu ya kuchumbiana, mimi na Nasib tumeamua kwa dhati kuachana," Zuchu alitangaza.

Aliongeza, "Huu ulikuwa uamuzi wa pande zote mbili, tuna mradi ujao kwa hivyo usishangae utakapotolewa."

Zaidi ya hayo, mwimbaji huyo mrembo mwenye sauti ya kusisimua alimtakia kila la heri Diamond ambaye pia ni bosi wake wa WCB katika shughuli zake zijazo.

Aidha, alidokeza kuwa sasa atazingatia uponyaji na kazi yake.

"Ninawaomba watu wangu wema kuwa na sapoti yenu isioisha kwani lengo langu kuu sasa ni uponyaji na kazi yangu. Wako mwaminifu, Zuchu," alisema.

Mastaa hao wawili wa bongofleva wamekuwa wakichumbiana waziwazi na kuonyesha mapenzi yao kwa takribani miaka mitatu iliyopita. Wamesafiri pamoja, wakapeana zawadi za bei ghali, wakabusiana hadharani, na kuoneshana mapenzi mengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved