Gloria Kyallo dada yake mwanahabari wa runinga Betty Kyallo amethibithisha kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Ken Warui.
Hata hivyo Gloria ameeleza kwamba licha mtafaruku uiloko na kukosana kwao bado wanaendelea kumulinda mbwa wao kwa pamoja kama ilivyokuwa hapo awali.
Swala hili la kuvunjika kwa mahusiano hayo ya muda mrefu lilijitokeza kwenye mahojiano kwenye akaunti ya Gloria ya Instagram.
"Mbona mliachana na Ken? Halafu huyo mbwa wenu mdogo mnasaidiana kulinda?" mfuasi wake mmoja kwenye mtandao wa Instagram aliuliza.
"Nimejibu swali hili kabla ya hapa na nimeshaliandika katika mtandao, sawa acha niseme tunasaidiana kumulinda mbwa, lakini kwa sababu mara mingi anammiliki yeye, sipati muda naye mara kwa mara."
Gloria Kyallo na mpeniziwe Ken Warui wamekuwa pamoja kwa muda mrefu, mapenzi yao wamekuwa wakiyaweka hadharani hasa katikaka mitandao ya kijami.
Swala la wawili hao kuachana bado halijajulikana wazi. Kwa upande wake Gloria Kyallo alidinda kuzungumzia jambo hilo huku akieleza kwamba kilicho katikati yao ni kusaidiana kumulinda mbwa wao mudogo.
Kyallo ambaye hakuweka wazi kuhusiana na maisha yake kwa sasa au uhusiano mpya alionekana kutojutia kuvunjika kwa mapenzi yao kuashiria kwamba huenda hayakumuacha na majeraha ya mapenzi.
Kutengana kwa wawili hao kuliacha mashabiki na wafuasi wao kwenye mitandao na mwitikio wa mchanganyiko.
Lakini swala la kuendelea kumulinda umbwa wao pamoja wakati wamekosana pia kunachora taswira tofauiti katika mapenzi yao ambayo yamedumu kwa muda mrefu.
Swala la wapenzi kutengana hasa watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii limekua likitokea mara kwa mara. Ila mara mingi chanzo hakiwekwi wazi.