
Kungwi ambaye ni msharu wa Mapenzi na dakitari katika taifa jirani la Tanzania sasa anadai kwamba mwanaume mwenye kitakimbi na tatizo kubwa kwenye ndoa yake.
Mwadada huyo amewataka watu wenye unene kupita kiasi hasa kitambi kufanya mazoezi ya kutosha ili kupnguza uzani jambo ambalo amesema linasaidi katika afya na pia kuleta amani nyumbani kwa wanandoa,
"Unene ni tatizo, unapoenda hosipitali kupimwa unaambiwa anza mazoezi. Unene ni kitu kibaya sana sio tu kwa mwanamke lakini mpaka kwa mwanaume, uko na kitambi utawezana na kazi ya ndoa. wanaume wenye vitambi wana vituko," aliteta Kungwi.
"Wanaume wenye kitambi wana maneno mengi, watajigamba utaona nitakachokifanya lakini kitambi kinamaliza kila kitu. Alafu sasa umukute mama ana kitambi na baba ana kitambi. Lakini kuna kitambi kizuri kile kidogo," alisema huku akitilia shaka watu wenye unene wa kupitiliza.
Mshauri huyo pia ameeleza kwamba ni vizuri sana kutafuta msaada wa dakitari ili kupata mawaidha wakati unaona umeanza kunenepa kupita kiasi. Pia amependekeza wanawake kumuona daktari baada ya kujifungu ili kusaidiwa kutokana na dhana kwamba kuna baadhi ya watu wanapojifungua unene huongezeka.
"Kuna wale wakizaa wanabadilika lakini siku hizi kuna uwezo wa kuvutwa mafuta kwenye tumbo kuna daktari wanafanya na tumbo linakuwa flati. Lakini sehemu za mwili kama vile mikono zinaweza zikapunguzwa kupitia mazoezi ya kutosha," alieleza.
"Mwanamke na mwanaume wenye miili mikubwa huwa na athari kwenye mahusiano. Ni vyema mwenyewe uwelewe tu kwamba hapa kuna tatizo. Ni vizuri zaidi kuchunga chakula unachokula na kutumia maji moto,"alaielza dakitari kungwi.
Ameongeza akisema kwamba mwanadada baada ya kuingi kwenye ndoa aendelee kufanya mazoezi na baadhi ya kazi sio tu kumuachia dada mjakazi.
"Wakati unakosa kufanya kazi na mazoezi, mwili unarelax. usimuachie msichana wa nyumbani kazi pekee. zingatia vyakula unavyotumia na mazoezi," alisema.