
MATOKEO ya historia ya ‘Google search’ kwenye simu ya mtuhumiwa yametumika kama Ushahidi mkuu katika kesi ya mauaji ya mwanamke ambaye alikuwa mpenzi wake.
Ty Vaughn, 31, kutoka jimbo la Texas
nchini Marekani sasa anashtakiwa upya kwa mauaji ya mpenziwe baada ya awali
uchunguzi wa kifo hicho kuonekana kama wa mtu kujitoa uhai mwenyewe.
Kwa mujibu wa jarida la PEOPLE, Vaughn alikamatwa
na kushtakiwa kwa mauaji mnamo Ijumaa, Machi 7, kuhusiana na mauaji ya Januari
ya Luis Banos mwenye umri wa miaka 27.
Mnamo Januari 14, maafisa wa polisi
walijibu katika jumba la ghorofa huko Baytown baada ya mpiga simu 911 - ambaye
baadaye alitambulika kama Vaughn - kudai kuwa amepata mchumba wake amekufa
kutokana na jeraha la risasi, taarifa hiyo inasema.
Ndani, polisi walimkuta Banos akiwa
amekufa na jeraha dhahiri la risasi na kumzuilia Vaughn kwa mahojiano.
"Wakati wote wa uchunguzi,
Vaughn alitoa taarifa zisizolingana,"
polisi walidai. "Baadaye wapelelezi walibaini sababu ya kifo kuwa
mauaji."
Vaughn sasa anashtakiwa kwa kumpiga
risasi Banos usoni na bunduki na baadaye kuonyesha mauaji kama mtu wa kujitoa uhai.
Hii ni baada ya kubainika kwamba
alitafuta mtandaoni ili kujua madhara yalikuwaje kwa "raia halali"
kumuua "mhamiaji haramu," kabla ya kifo cha Banos, kulingana na
waraka huo.
Nyaraka za mahakama zilizotajwa na ABC13
zinasema kwamba polisi waligundua kuwa aliwahi search kwenye mtandao wa Google,
"Je, ninaweza kumuua binadamu haramu?"
Kulingana na Fox 26, nyaraka za mahakama
zinaonyesha Vaughn baadaye aliwaambia polisi kwamba mchumba wake "hakuwa
na hadhi ya kisheria."
Polisi wanadai Vaughn alikuwa anajaribu
"kupunguza au kudharau hadhi au thamani ya (Banos')," kwa kujadili
hali yake ya uhamiaji, ripoti za San Antonio Express-News, zikinukuu hati ya
kiapo ya upekuzi. Banos aliripotiwa kuwa mzaliwa wa Mexico.