logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Bonez azungumzia madai ya mkewe Kamene Goro kuiba mume wa wenyewe

“Sijawahi kuoa. Saa hi indo nimeoa mara ya kwanza kisheria.Kuna ile ya come we stay na kuna ndoa rasmi,” Bonez alisema.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri25 July 2023 - 09:40

Muhtasari


•Bonez alifichua alikuwa katika uhusiano wa miaka miwili na mwanamke mwingine kabla ya kukutana na Kamene Goro.

•Bonez alimtetea mkewe kuhusu madai ya ‘kumuiba’ kutoka kwa mwanamke mwingine akieleza kuwa tayari alikuwa ametengana na aliyekuwa mpenzi wake.

Kamene na mumewe DJ Bonez

Mume wa mwanahabari Kamene Goro, David Kamau almaarufu Deejay Bonez amefunguka kuhusu historia yake ya uchumba.

Wakati akizungumza kwenye podikasti ya Kamene na Obinna, mcheza santuri huyo alifichua kwamba alikuwa katika uhusiano wa miaka miwili na mwanamke mwingine kabla ya kukutana na Kamene Goro.

Wakati uo huo, alipuuzilia mbali madai ya kutelekeza familia yake kwa ajili ya Kamene Goro huku akifichua kuwa uhusiano wake na mzazi mwenzake ulikuwa umevunjika hata kabla ya yeye kuchumbiana na mwanamke aliyetangulia mbele ya mtangazaji huyo wa zamani wa redio.

“Niko na baby mama. Lakini niko na ex baada ya baby mama,” Deejay Bonez alisema.

Aliendelea kueleza, “Hiyo ndo kitu watu hawajawahi kuelewa. Ndio maana watu huwa wananitukana ama wanatutukana. Nilikuwa na ex kwa miaka miwili baada ya baby mama, Kisha Kamene akaja.”

Bonez alimtetea mkewe kuhusu madai ya ‘kumuiba’ kutoka kwa mwanamke mwingine akieleza kuwa tayari alikuwa ametengana na aliyekuwa mpenzi wake.

Mcheza santuri huyo pia aliweka wazi kuwa amekuwa kwenye ndoa mara moja tu maishani, ambayo ni ndoa yake ya sasa na Kamene.

“Sijawahi kuoa. Saa hi indo nimeoa mara ya kwanza kisheria. Kuna ile ya come we stay na kuna ndoa rasmi,” Bonez alisema.

Bonez alidokeza kuwa mwanaume kuwa na mtoto na mwanamke fulani haimaanishi kuwa walikuwa katika ndoa.

“Kamene hajawahi kunyang’anyana mume. Hata ex wangu hakuwahi, nilikuwa nimemweleza kila kitu,” alisema.

Wiki jana, Kamene alifichua alikutana na mumewe wakati wa ziara ya Pwani, na kwao, haikuwa  mapenzi mwanzoni.

“Tulikutana Mombasa, Hatukupendana mwanzoni. Wakati huo rafiki wa Bonez alikuwa na sherehe ya siku ya kuzaliwa, ana klabu. Baadaye nilirudi katika klabu hiyo na mtangazaji mwenzangu wa zamani. Bonez aliwahi kusema mimi ni mzinzi. Nilikuwa mdogo wakati huo." alisema.

Kamene alisema amemfahamu Bonez tangu 2015

"Alinichukia, hatukuwahi kuongea. Mnamo 2020 Desemba nilikuwa na rafiki yangu. Tulitua na tukapelekwa Serena Hotel. Tukaamua kukodisha jahazi, na tuliambiwa tunaweza kupata DJ ndani, kwa hivyo tukakodisha nafasi ya jahazi hilo.

Tulikuwa wawili tu. Sherehe ilianza. Muda si muda nikamuona DJ Bonez, tukazungumza na nikarudi kuongea na marafiki zangu."

Rafiki yangu alikuwa amechukua power bank yangu, yeye (DJ Bonez) alipiga simu na kabla hajasema chochote alichotaka, nilimuelekeza kwa mtu mwingine (Terry). Nilidhani anataka power bank," alisema

Baada ya hapo, alikuwa akija kila siku hotelini na tulikuwa tukijivinjari."

Bonez alisema muda huo wote alikuwa na namba ya Kamene kwani walikuwa kwenye kundi fulani pamoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved