logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya wakaazi wa Juja kung'ang'ania mikate na juisi kufuatia ajali iliyohusisha lori mbili

Wakazi walikimbia kuchukua mgao wao wa bidhaa za bure  baada ya lori mbili zilizokuwa zimebeba vyakula kugongana kwenye barabara kuu ya Thika.

image
na Samuel Maina

Burudani26 March 2024 - 06:31

Muhtasari


  • •Wakazi walikimbia kuchukua mgao wao wa bidhaa za bure  baada ya lori mbili zilizokuwa zimebeba vyakula kugongana kwenye barabara kuu ya Thika.
  • •Baadhi ya Wakenya wamewakosoa waliojisaidia kwa bidhaa hizo za bure, wengine wakitamani wangekuwepo na wengine hata kushangaa jinsi tukio hilo lilivyotokea.
waling'ang'ania mikate na juisi baada ya lori mbili kugongana Jumatatu.

Wanamitandao wa Kenya wameendelea kutoa maoni mseto baada ya wakaazi wa mji wa Juja kung’ang’ania mikate na juisi kufuatia ajali iliyohusisha lori mbili Jumatatu mchana.

Video za tukio ambazo zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha drama kubwa katika mji huo wenye shughuli nyingi katika kaunti ya Kiambu huku wakazi wakikimbia kuchukua mgao wao wa bidhaa hizo za bure  baada ya lori mbili zilizokuwa zimebeba vyakula kugongana kwenye barabara kuu ya Thika Superhighway.

Ajali hiyo iliyotokea katikati mwa mji wa Juja ilisababisha kumwagika kwa mikate na vinywji vya aina mbalimbali barabarani, na kuvutia umati mkubwa wa watazamaji na wapita njia, kila mtu akitafuta kutoka na kitu.

Katika video hizo, baadhi ya wakazi wanaonekana wakitazama huku wengine wakikimbia na mikate mingi na juisi kadri ya uwezo wa mikono yao.

Maafisa wa polisi walijaribu kuzuia hali hiyo lakini  kufikia wakati mambo yalipoa, vyakula vingi vilikuwa vimechukuliwa.

Wakenya wameendelea kutoa maoni yao kuhusu hali hiyo, wengine wakiwakosoa watu waliojisaidia kwa bidhaa hizo za bure, wengine wakitamani wangekuwepo na wengine hata kushangaa jinsi tukio hilo lilivyotokea.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii;

Lord Abraham Mutai: What are the odds for such an accident 🤔. These are Juja residents scrambling for bread and juice after an accident involving a lorry carrying bread and another carrying  juice along Thika Road. And, must we always loot from accidents scenes?

Vu.vah: Leo macomrades atleast wataonja Ribena.

King.mungai: Waaah, evebody’s childhood dream.

Tv.mounting_: Yes, shame on them. Rather than helping, they take. Mankind.

Kylkihia: And we complain when politicians steal from us.

Kiokod37: Those saying shame on you, hiyo stock hakuna mahali itauzwa ata ikiwa rescued na insurance so wananchi wafurahie.

Kangui_benson: Kila mtu anajua shida zake, stop judging.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved