Muundaji maudhui za kidijitali na mpiga picha Faustine Lipuku maarufu kama Baba Talisha amefichua kwamba amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa kwa wiki moja.
Baba Talisha anasema kwamba ameenda hospitalini na kushauriwa kupumzika baada ya vipimo kuonyesha kuwa kila kitu kiko sawa.
“Imekuwa wiki moja na zaidi, dawa za kutuliza maumivu hazifanyi kazi, nilienda ct scan na inaonyesha kila kitu iko sawa, lakini nilishauriwa nipumzika, nikanywa dawa za neuro ili kunitia ganzi lakini hakuna inayofanya kazi. Jamani msiniroge, nitaachia nani mtoto?”
Anaeleza kwamba maumivu ya kichwa yalianza alipopoteza vitu vyake kwenye gereji na gari lake kuharibiwa. Kinachomtia wasiwasi ni hakuna atakayebaki na mwanawe Talisha ikiwa mambo yataenda mrama. Pia ameshindwa kufanya kazi kama kawaida kwa sababu ana msongo wa mawazo kuhusu kazi na bintiye.
“Kwa kawaida huwa nina tatizo la wasiwasi tangu nilipopoteza vitu vyangu kwenye gereji na gari langu kuharibiwa, haijawahi kuwa sawa. Hapo ndipo kichwa kilianza kuniuma. Nilidhani ni maumivu ya kichwa nyepesi lakini hata baada ya kutumia dawa kali za kutuliza maumivu, hakuna kilichobadilika. Yaani nimeteseka na hii kichwa kwa wiki nzima. Karibu nifikirie naenda bana. Na hakuna kitu mbaya kama kuoverthink juu sasa unafikiria tu mtoto na kazi unable to work vile nimekuwa na bado hata the worst ikihappen yaani Talisha atabaki hivyo tu. Ile stress inaninyorosha sahii,”
Anaendelea na kusema kuamka kila siku na kutojua kinachokusumbua kiafya sio jambo nzuri hata kidogo.
“Kuamka kila siku kujisikia kufadhaika, kukata tamaa, kuwa mgonjwa na hujui kinachoendelea ni mbaya haswa Ikiwa hujui hata la kufanya yaani uko mnyonge. Dawa hakuna kitu zinafanya. Hulali, stress zinakunyorosha tu, hakuna anayeweza kuelewa kinachokusumbua,”
Mwezi uliopita Baba Talisha alieleza jinsi alivyopeleka gari lake gereji ili lirekebishwe na kupigwa na butwaa baada ya kupata limeharibiwa na hata baadhi ya vitu vyake kuibiwa.