Mtayarishaji wa maudhui za dijitali Thicky Sandra
amesema kuwa hana mpango wa kufanyiwa upasuaji wa urembo ili kubadilisha muonekano
wake wa mwili.
Kupitia kwenye chaneli yake ya YouTube, alizungumzia
mada hiyo baada ya kuibuliwa na mmoja wa wafuasi wake kwenye mitandao ya
kijamii wakati wa kipindi cha maswali na majibu kilichofanyika kwenye
Instagram.
Kulingana na Sandra, anaupenda mwili wake jinsi ulivyo.
Aidha alifichua iwapo angefanyiwa utaratibu angepata moja inayolenga eneo la
tumbo lake ili kupunguza ukubwa wa tumbo ila bado yuko sawa na jinsi tumbo lake
ilivyo.
“Ikiwa ni upasuaji wa kurekebisha mwili wangu na mimi
mwenyewe, ningesema hapana. Ikiwa ningefanya kitu, ningefanya wood therapy ili
kupunguza tumbo langu,”
Aliendelea na kusema kitu kilicho kwa mwili wake
ambacho angefikiria kubadilisha ni stretch marks ambazo anasema ziko sehemu
mbalimbali mwilini mwake. Lakini hata kuhusu hilo alisisitiza kuwa bado
hatafanya upasuaji.
"Lakini nataka tu kuondoa stretch marks. Nina
stretch marks nyingi sana kwenye mikono, tumbo, mapaja na nyash. Nisingefanya
upasuaji lakini laser. Hicho ndicho kitu pekee ambacho ningetaka kifanyike kwa
mwili wangu,” Sandra alisema kwenye video aliyowekwa kwenye chaneli yake ya
YouTube.
Kuhusu ikiwa anapanga kupata watoto Sandra alisema
kwamba anapanga kupata watoto lakini miaka kumi na zaidi kutoka sasa.
“Ndio, lakini labda baadaye maishani, kama miaka 10-15
kutoka sasa. Hapo ndipo ninapanga kupata watoto,” Sandra alisema.
Sandra pia alifichulia wafuasi wake anachofanya
anapokumbana na haters ambao hukejeli maumbile yake.“
Kadiri wanavyoniburuta chini ndivyo ninavyoinuka juu,” alisema.
Anasema ukiwa na haters inamaanisha unafanya kitu
kizuri tofauti na kukosa haters kwani inamaanisha hakuna kile unachofanya.