Usuli na historia ya msanii Hussein Machozi.
Hussein Rashid Juma alimaarufu Husein Machozi alizaliwa
mnamo tarehe 6 Oktoba,1986 Manyoni Singida Tanzania.
Hussein Machozi ni mwanamuziki vilevile ni mtunzi wa nyimbo
za kisanaa,Hussein alianza kuimba akiwa mwana mdogo alikuwa akimwimbia mama yake huku
akimuarifu kuwa ipo siku atakuwa msaanii
taajika.
Alipofika umri wa ujana Hussein alianza kujihusisha katika
makongamano na warsha mbalimbali za muziki huku akiwatumbuiza wageni na watu
mbalimbali,alizidi kikinoa makali kipaji chake kwa kuendelea kuandika nyimbo na
kujituma zaidi.
Kipaji chake kilipozidi kutamba na kung’aa zaidi Hussein alitambulika nchini Tanzania na
kuanza kuimba kwa mvuto wa hali ya juu na akawa anawavutia mashabiki wengi nchini
na hata katika mataifa ya Nje kama Kenya na Uganda.
Nyota yake iling’aa pale alipokutana na wanamziki wa bendi
ya Sauti Sol na akashirikiana nao na kutoa kibao cha Utapenda kibao
mbacho kiliteka angaa na kuwavutia mashabiki wengi,wimbo ambao aliujumuisha
katika alibamu yake ya kwanza.
Hatimaya alitoa kibao kimoja kwa jina ‘’Kafia Ghetto’’kibao
ambacho kilihanikiza ukanda wa Afrika Mashariki kwa jumla na kummegea sifa
belele,kibao hicho kiliweza kuchezwa katika idhaa za Redio Tanzania.
Husein Machozi Kutokana na mtindo wake wa kuimba na kughani
mashairi kwa namna ya kipekee ulimpevusha na kumweka katika Daraja ya magwiji
wa sanaa ya muziki, hadi leo yeye ni msanii mzuri tena wa kuigwa katika taasinia ya mziki kwa kuimba
vibao motomoto tena aina ya Bongo fleva.
Hussein aliwahi toa vibao vingi vikiwemo kwa Ajili yako,Nipe
sikuachi,Full Shangwe,Addicted ,Unanifa, za Mwizi 40 na Jela kibao ambacho
kilisisimua umma na mashabiki wake kutokana na utunzi imara na ubunifu wa hali
ya juu.
Kibao heri nirudi Jela kilikuwa miongoni mwa vibao ambavyo
vilifanya vyema zaidi katika alibamu ya msanii
Husseni na kumpandisha kisanaa, hivyo akawa ni mwanamziki ambaye aliyetambulika
na kuheshimiwa sana.
Hussein Machozi kwa muda mrefu amekuwa kimya lakini kutokana
na mashabiki wake kushikwa na uchu wa kutaka kumuona akichemka tena na kuachilia
magoma ya kipekee wameshinda wakimchokoza wakisema kuwa wangependa kusikia
kibao kipya mwaka huu.
Kulingana na dalili za bwana Hussein katika mitandao ya
Kijamii japo hajadokeza ni lini ataachilia bonge la kibao kipya ila ameonyesha dalili
za kuwajibu mashabiki wake kuwa wawe na Subira mambo mazuri yaja.