Msanii Zuchu na safari yake kimziki
Zuhura Othman Soud alimaarufu Zuchu ni msanii wa kike kutoka Tanzania alizaliwa mnamo tarehe 22 Novemba,1993.
Zuchu ni mwanamziki wa kipekee anayeimba miziki aina ya Bongo na yuko katika usimamizi wa WCB ambayo inamililkiwa na msanii Diamond.
Zuchu ni mwanawe msanii wa taarabu ambaye ni taajika bi Khadija Kopa na mzee Othman Soud ambaye naye alikuwa mtunzi Hodari wa nyimbo.Zuchu alizaliwa katika familia ambayo iliinukia katika misingi ya sanaa ya mziki.
Kupitia kwa mamake Zuchu alipata fursa ya kukutana na nguli Diamond ambaye ni mwasisi wa brandi ya WCB ambapo alijiunga na lebo hiyo mnamo mwaka wa 2016,katika safari yake ya maisha Zuchu alianza kuimba akiwa mdogo wakati ambapo alishirikiana na mamake katika wimbo mauzauza.
Mnamo mwaka wa 2022 Zuchu alikuwa mwanamziki wa kwanza kufikisha mashabiki milioni 100 kwenye mtandao wa Boomplay jambo ambalo lilimpa sifa na hadhi ya kuweza kujulikana katika viwango tofauti na kupanua wigo wake kimziki.
Baadhi ya vibao ambavyo vimemkweza na kumuweka Zuchu katika ramani ya kimataifa ni Kwikwi,Utaniua,Fire,Mwizi,Walewale,Naringa,Mwambieni na kadhalika,kutokana na mtindo wa kipekee wa msani huyu ambaye ni kinda katika tasinia hii ya mziki ameonekana kufanya vyema na kutwaa mataji na tuzo nyingi.
Mnamo mwaka 2023 Zuchu aliimba kibao cha Utaniua wimbo ambao ulisherekewa na kufurahishwa sana na mwanahabari wa Tanzania Charles Majanja ambako alipenda na akakitukuza na kumhongera sana Zuchu kwa kuonyesha ubunifu na umbuji wa hali ya juu katika utunzi na kuimba kwake.
Baada ya kuzindua kibao cha Napambana mwaka huo wa 2023 na kutoa video kali sana ambayo ilivutia na ikafurahisha sana hadi ikampa na kufanya nafasi yake akawa katika viwango tofauti jambo hilo liliweza kufanya wimbo wake kurodheshwa na kuwa nambari 8 katika urodha ya nyimbo bora nchini Tanzania.
Mashabiki wa Zuchu wamekua wakimhusisha kimahaba na msanii Diamond ikisemekana kuwa wawili hao huwa wanaendesha ukuruba kimapenzi chini ya zulia madai ambayo kwa mara moja Zuchu alijitokeza na kukiri kwa kuchapisha katika mtandao wake wa Instagram jambo ambalo lilishusha pumzi na kufanya mashabiki kutulia na kukubali mahusiano kati yake na Simba Nasibu.