
Mwanamziki Yusuf Kulungi maarufu Mbosso Khan amezungumzia hali yake ya afya baada ya kutoka hospitalini siku chache zilizopita.
Mwanamziki huyo alifanyiwa oparesheni ya moyo, na kwenye mahojiano na stesheni ya radio moja huko Tanzania alieleza kwamba alikwenda kutafuta matibabu, ila haikuwa kuumwa.
"Maradhi ya moyo nilikuwa nayo muda mrefu tangu nizaliwe, na watu walisema ni maradhi ya kurithi, wakasema hata marehemu bibi yake alikuwanga vivyo hivyo. Kwa hivyo hata mimi nilikuwa nimejiwekea hiyo imani kwamba huu ni ugonjwa wa kurithi," alifunguka Mbosso.
Mbosso pia aliweka wazi dalili ambazo zilikuwa kwake kwa muda mrefu hivyo kuchangia pakubwa kwake kutafuta suluhisho katika afya yake.
"Mikono yangu ilikua inatetemeka sana, wakati mwingine napata maumivu ya moyo sana hasa nikitoka kulala au nikitoka kuperfom nilikua najisikia mchovu sana na maumivu makali. Pia nilikua najitahidi kufanya mazoezi mara kwa mara, nilijaribu sana kufuata ushauri wa madaktari, nilikua natafuta ushauri kwao mara kwa mara na wakanishauri nipunguze vyakula vyenye mafuta. madaktari walinieleza kwamba nina dalili ya mishipa yangu kufungana kutokana na mafuta mwilini," Mbosso aliweka wazi.
"Kiukweli ilinibidi niachane na chakula chenye mafuta, nilikuwa nakula chakula ambacho hakikaangwi. Damu yangu pia haikuwa inazunguka vizuri. Chakula chenye chumvi wala sukari sikuwa natumia, kidogo ilikuwa ngumu lakini ilibidi nijitahidi na ilinisaidi," mwanamziki huyo aliendelea kueleza.
Kwenye mahojiano Nyota huyo wa bongo alitoa shukrani zake kwa Rais wa muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu kwa kuanzisha mpango wa wasanii kupimwa akisema kwamba huo ndio ulikuwa mwanzo wake yeye kuendelea kuafuatilia afya yake pamoja na matibabu.
"Mwanzoni Mama Samia Suluhu Hasani alisema wasani wote twende tukapimwe kupitia tasisi ya Jakaya, ugonjwa wa Moyo. Mimi nilikuwa kama sitaki ila nikaamua acha niende nione itakuwaje nikajipata nina shida ya umeme wa moyo na wakaniahidi kunisaidia," aliongeza
Nyota huyo aliwataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kwani yeye alienda kutibiwa wala haikuwa kuumwa.
"Lile tukio mliloliona mimi nilienda kutibiwa sio ugonjwa eti nimezidiwa. ni rasimi kwamba nimepona, ata ukinipa shamba nalima. kitu ambacho bado nakitunza ni kuhusu vyakula maana ni mapema sana naeza kujiweka kwenye hatari," aliweka wazi mwimbaji huyo mwenye kibao cha penzi lina raha yake.