logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Ibrah afichua kwamba ameoa na ana mke

Ibraah alifichua haya akiwa kwenye mahojiano na wanahabari walipotaka kujua vipi kuhusu mahusiano yake.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako24 February 2025 - 08:56

Muhtasari


  • Akizungumza ameeleza kwamba mahusiano yake na mchumba wake sio ya siri lakini ni ndoa kabisa na wala hana wazo la kurudi nyuma.
  • "Nimemficha wapi, wewe ulitaka umuone wapi, mke ulidhani ni nini umukute kokote, yuko vizuri wewe ulimuona wapi," alisema.

Mwanamziki wa bongo Ibraah amefichua kwamba yeye tayari ameoa na ana mke ambaye wako katika mahusiano mazuri.

Ibraah alifichua haya akiwa kwenye mahojiano na wanahabari walipotaka kujua vipi kuhusu mahusiano yake ambayo siku zote hajaweka wazi, huwa faraghani kinyume kabisa na wanamuziki wengine.

Akizungumza, alileza kwamba mahusiano yake na mchumba wake sio ya siri lakini ni ndoa kabisa na wala hana wazo la kurudi nyuma.

"Mimi sio leo naambia watu nimeoa, ata mnavyoniuliza nawaambia kwamba nimeo nina mke, sio kwamba ni mara yangu ya kwanza nakutana na yeye mtaani, mke wangu kabisa, ndoa kabisa," Ibraah alifichua kuhusu ndoa yake.

Pia alieleza kwamba yeye hajutii kumficha mkewe na ana sababu zake ambazo anaamini mbona hajaamua kumueka mpenzi wake hadharani  kama wanavyofanya wasanii wengine.

"Nimemficha wapi, wewe ulitaka umuone wapi, mke ulidhani ni nini umukute kokote, yuko vizuri wewe ulimuona wapi" mwanamziki huyo alisema.

Msanii huyo wa muziki wa bongo fleva pia aliweka wazi kwamba mkewe ni mzaliwa wa Burundi ila walikutana alipokuwa nichini Tanzania wakati yeye alikuwa akiendelea na shughuli zake za kimuziki.

"Shemeji yenu nilimtoa Burundi, ila tulikutana Hapa Tanzania kwenye shughuli zangu za kimuziki, alipofika Tanzania, mimi sikuwa karibu nilikuwa Dar es salaam Mwanza. Sasa hivi tumekaa naye unaenda mwaka wa tatu." nyota huyo wa Tanzania alisema.

Ibraah kwa upande wake anaamini kwamba kuwa na umaarufu hauhusiani na maamuzi ya ndoa, huku pia akieleza kwamba sio eti hakuona msichana mzuri Tanzania ndipo akaamua kuoa inje ya nchi lakini Mapenzi humea popote na hayachagui.

"Umaarufu wangu, nadhanu umaarufu hauhusiani na mahusiano kwa sababu mimi ni kijana ambaye kama nikucheza nishacheza na sina tamaa ya kuendelea kufanya hivyo vitu. kwa hivyo lazima nitafute mtu wa kumuheshimisha kidogo. Kuhusu swala la kuto oa hapa nchini ni mapenzi, mapenzi yakitokea yanatokea popote," msanii huyo mwenye kibao maarufu 'Nimependa' alieleza kwa umakini.

Ibraah ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri katika miziki ya bongo na amekubalika sio nchini Tanzania bali hata inje ya nchi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved