Produsa maarufu wa muziki nchini Tanzania Joachim Marunda Kimaryo maarufu Master J amepinga kauli kwamba mwanamziki Diamond Platinumz alimsaidia Mwanamziki wa Konde Gang Harmonize kusimama katika tasinia ya muziki.
'Haya maneno ya kusema kuwa umemsaidia mtu, umemsaidia mtu saa ngapi, huyo Naseeb yeye watu ambao amewasainii, wote hawasaidii. Hizo ni shughuli za kibiashara tu. Mikataba ipo, mimi nitawekeza kiasi fulani," alisema Master J.
'Turekodi audio, tushooti video, na kufanya marketing and promotion. pesa zikipatikana wewe utachukua asilimia fulani na lebo itachukua kiasi fulani, msaada uko wapi? Ukitaka kuchomoka kabla ya kile nilichoeekeza hakijarudi, nilipe," alifafanua zaidi Muundaji huyo wa Muziki, Master J.
Kwa upande wake pia alieleza kwamba kumsaidia mtu kwenye tasnia ya mziki ni kumfanyia kazi mtu kisha umpe kazi na faida ya kazi hio ni yake lakini sio kuekeza nyote.
"Kumsaidia mtu ,ni kumsaidia kushooti video na audio kisha umwambie mzigo ndio huu hapa. Huo ndio msaada. Lakini hakuna msada kwenye lebo. Kwani mtu atoe hela yake bure. Mtu akusaidie milioni 50 au milioni 100, bure," alisema Mater J kwa kutilia shaka.
Master J kando na kuwa mutayarishaji wa muziki pia ni jaji katika shindano la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki nchini Tanzania maarufu kama Bongo Star Search.
Master J amewahi kupata tuzo ya 'Kili Music Award' mara mbili, mwaka 2004 na 2006. Master Jay ana uwezo mkubwa sana wa utengenezaji wa muziki. Anamiliki studio tatu tofauti, moja ya muziki wa kwaya, moja ya Bongo fleva na nyingine ya muziki wa Dansi.