
Mwanamziki wa bongo Tanzania Raymond Shaban maarufu kwenye kazi yake ya muziki kama Rayvanny amesisitiza kwamba msimamo wake katika maswala ya siasa haufai kumutenganisha na mashabiki wake kwenye tasinia ya muziki.
Mwanamuziki huyo amesema kwamba msimamo wake katika maswala ya siasa au dini haufai kuwa na athari kwenye muziki.
"Mimi kuchagua chama ambacho nakitaka au uongozi ambao ninauona upo sawa ni maamuzi yangu. Shabiki yangu ananiunga mkono muziki wangu, sasa itikadi za vyama au sijui dini, haziwezi kututenganisha kutuweka kwenye makundi, hapana, hatufanyi hivyo hasa Tanzania. Mtu anajua wewe ni CCM na yeye labda ni chama kingine lakini bado anaunga mkono mziki wangu," alieleza kwa umakini msanii Rayvanny.
Mwanamuziki huyo pia ameeleza kwamba ili kufanikiwa zaidi kimuziki unafaa uweke uhusiano mwema na wanasiasa maana pia ni baadhi ya watu ambao wanaongeza mapato kwa kazi ya muziki.
"Panaweza pakawa na mkututano wa kisiasa, lakini wakaitwa pale wasanii kutumbuiza, wakaimba kwenye mkutano wa chama chao na wakapata chochote kitu, sasa hiyo kwa upande mmoja au mwingine unanufaika," alieleza zaidi.
Rayvanny amekanusha madai kwamba uhusiano wake na bosi wake wa zamani kwenye lebo ya Wasafi Diamond platinumz umezorota. Ameeleza kwamba wangali marsafiki wakubwa na wanazungumza kwenye simu. Pia amefunguka kwamba aliondoka wasafi kwa uzuri na alifurahia akiwa huko na wala hakuna kilichokuwa kibaya.
"Maisha yalikuwa mazuri, unajua unapopata chochote, unapopata riziki, mkono unaenda kinywani hapo uko sawa. 'Niliamua kutoka' sababu ni ukuaji, huwezi ukakaa nyumbani miaka yote. Ukikaa hata kama ni kuzuri utasemwa tu, huyu naye ana miaka 50 bado yupo nyumbani," aklifichua msani huyo wa bongo.
Mwanamziki Rayvanny pia alipinga tetesi kwamba alikua ananyanyaswa kimuziki wakati angali kwenye lebo ya Wasafi na kueleza kwamba hata mpaka sasa mahusiane yake na Diamond bado ni mazuri.
"Hapana sio kweli, sisi ni familia, yeye 'Diamond' ni kaka yangu, yaani tunaongea vizuri sana. Jana tu juzi tumeongea karibu saa zima," alikanusha tetesi.
Rayvanny ni msanii wa muziki, mwandishi wa nyimbo, na Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya rekodi ya 'Next Level Music'.