logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP: Mtangazaji Mutahaba kufariki akipokea matibabu Afrika Kusini

RIP: Mtangazaji Mutahaba kufariki akipokea matibabu Afrika Kusini

image
na

Michezo02 October 2020 - 00:37
Ni machozi na kifo kilicho wakumba familia ya mtangazaji maarufu Ruge Mutahaba, hii ni baada ya kumpoteza mwanahabari huyo akiwa katika matibabu nchini Afrika Kusini.

Mutahaba aliweza kupumua pumzi yake ya mwisho Jumanne akiwa katika hospitali moja mjini Afrika kusini.

Mtangazaji huyo maarufu alikuwa mwelekezi wa kipindi cha mikakati na mipango ya maendeleo (strategy and programme development) katika runinga ya Cloud Media Group.

Aliweza kufariki baada ya kupambana na ugonjwa wa kushindwa kwa figo kwa muda mrefu.

Wakati habari za kifo cha punde chake mwanahabari Ruge Mutahaba ziliweza kusambaa sana katika mitandao ya kijamii watu wanaofahamika na watu maarufu waliweza tuma rambirambi zao.

Rais John Pombe Maghufuli aliweza tuma rambirambi zake kwa familia kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter na kusema..

“I have received with shock information about the death of Ruge Mutahaba,” Aliandika Maghufuli. Aliweza kumjulisha Mutahaba kama kijana wake.

Haikuchukua muda mashabiki wasanii na marafiki zake waliweza pia kutuma rambirambi zao kupia mtandao huo.

@MariaSTsehai: Rest in peace our brother Ruge...Your contribution to the media industry has left an indelible mark!Pumzika kwa amani.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved