Shambulio la angani la serikali ya Syria uliolenga msafara wa kijeshi wa Uturuki uliokuwa ukielekea katika eneo linalotawaliwa na waasi kaskazini mwa Syria limesababisha vifo vya raia watatu, Uturuki imedai.
Watu wengine 12 walijeruhiwa katika shambulio hilo katika mkoa wa Idlib siku ya Jumatatu kulingana na wizara ya ulinzi ya Uturuki.
Mamia ya raia wameuawa kutokana na hilo na kuna hofu kwamba wengi watafariki iwapo hali itaendelea kuwa mbaya.
''Hii ndio hatari inayotukabili kwa sasa'', alisema Jan Egeland kutoka baraza la wakimbizi la Norway akizungumza na BBC.Kwa miaka kadhaa sasa tumeonya kuhusu hatari inayoikabilia Idlib , ambapo hakuna mahala pa kutorokea kwa raia milioni 3.
Kuna wapiganaji wabaya mjini humo. Lakini shambulio la jumla katika eneo hilo pamoja na lile lililomkabala la kaskazini mwa Hama litamaanisha kwamba watoto milioni moja wataathiriwa na vita hivyo na hicho ndicho tunakiona kikifanyika
Uturuki inayounga mkono baadhi ya waasi na sio wote ina majeshi yake Idlib kama mojawapo ya makubaliano na Urusi mwaka uliopita.
Kulingana na Naji Mustafa , msemaji wa waasi wa National Liberation Front msafara huo ulikuwa ukielekea katika mojawapo ya vituo vyake vya uchunguzi na walinzi wakati shambulio hilo lilipotokea,
Mwandishi wa AFP ambaye aliuona msafara huo anasema ulishirikisha magari 50 ya kijeshi , matano kati yao yakiwa vifaru.
Uturuki imesema kuwa shambulio hilo linakiuka makubaliano ya mwaka uliopita huku kisa hicho kikizua hofu kuhusu makubiiano ya moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa nini shambulio hilo lifanyike?
Baada ya miaka minane ya vita , serikali ya Syria inajaribu kuyakomboa maeneo yanayodhibitiwa na waasi.
Vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Urusi , viliripotiwa kuingia eneo la kaskazini magharibi la Khan Sheikhoun siku ya Jumapili.
Eneo la Khan Sheikhoun ambalo lilishambuliwa na gesi aina ya sarin mwaka 2017 lipo katika barabara kuu inayounganisha Damascus na Aleppo na ni eneo muhimu la kimkakati kusini mwa mkoa huo.
Iwapo litakombolewa , itamaanisha kwamba utawala wa Syria umefanikiwa kulizunguka eneo linalodhibitiwa na waasi upande wa kusini ambalo linashirikisha kituo cha uchunguzi cha Uturuki katika mji wa Morek.
Bwana Mustafa alisema kwamba msafara huo ulikuwa unaelekea Morek.
