logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Lionel Messi! Mambo 10 usiyoyajua Kumhusu bingwa wa soka duniani

Lionel Messi! Mambo 10 usiyoyajua Kumhusu bingwa wa soka duniani

image
na

Habari02 October 2020 - 03:30
Mu Argentina Lionel Messi alituzwa kama mchezaji bora zaidi wa soka katika tuzo za FIFA kwa mara ya 6 Jumatatu hii.
Alimpiku difenda wa Liverpool Virgil van Dijk na  Cristiano Ronaldo ambaye amewahi shinda tuzo hilo mara tano. Mshambulzi huyu anayevalia jezi nambari 10 ametamba na kupokea aina zote za tuzo za soka ulimwenguni.

 Messi alisajiliwa na klabu ya Barcelona akiwa na umri wa miaka 13.
Ilivyo sasa, Messi ni kati ya wachezaji wa kandanda wanaopokea kitita kikubwa cha mshahara, ikisemekana kuwa anapokea mshahara wa Sh 64.5 milioni kila wiki. Wasilojua mashabiki wengi ni kuwa mchezaji huyo aliugua ugonjwa mbaya sana akiwa mchanga.
Messi aliripotiwa kuwa na upungufu wa homoni ya ukuaji wa binadamu (Growth Hormone Deficiency).
Homoni hii ni muhimu kwani inachangia binadamu kuongeza kimo. Aidha, ukosefu wa homoni hii hufanya sehemu za uzazi, hasa kwa wanaume kusinyaa.
Hata hivyo aliposajiliwa na Baselona, klabu hiyo iliamua kugharamia matibabu yake kama sehemu ya mkataba wake. Alipewa matibabu ya kuzidisha homoni zake za ukuaji miguuni ili kuongeza kimo chake. Gharama ya matibabu yake ilikuwa zaidi ya $1,500 kila mwezi na alipokea kwa kipindi cha miaka 3 mfululizo.

Chakula anachokipenda huyu Messi tangu utotoni ni  aina ya Milanesa Napolitana. Chakula hiki ni maarufu sana katika nchi za Argentina na Urugwai. Hutayarishwa kwa jibini, vitunguu, nyanya pamoja na viungo vinginevyo. Pia anapenda nyama aina ya schnitze.

Messi hapendi kupiga simu! Yeye hutuma ujumbe mfupi au WhatsApp kama njia rahisi ya mawasiliano. Ni nadra sana yeye kupiga au kupokea simu isipokuwa wakati wa dharura.

Yeye ni mchezaji hodari wa PlayStation. Wakati hayupo uwanjani au pamoja na familia yake, yeye hutumia muda wake kujiburudisha kwa mchezo wa PlayStation.

Anapenda sana kuchana chale au tattoo.  Uso wa mama yake Messi umechorwa katika bega lake la kushoto. Pia amechora jina la mwanawe katika shavu la mguu wake. Hii ni ishara kwamba anaipenda na kuithamini familia yake sana.

Ijapokuwa Messi ni raia wa Uispania, ana urithi wa utamaduni katika mataifa mbali mbali. Baba yake alihama kutoka Italia huku mama yake akitoka nchi ya Lebanoni. Pia baadhi ya jamaa zake huishi kule Uingereza.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved