Bukeko aliaga dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi huku akizikwa na kupewa heshima zake za mwisho Jumatatu, ni hafla ambayo ilihudhuriwa na familia, jamaa na marafiki wake wa karibu.
Mama Nyaguthii ambaye aliigiza kwenye kipindi cha Papa Shirandula. bado hajaamini kifo cha Bukeko huku akisema bado hajafahamu jinsi ya kuendelea na maisha yake bila Papa Shirandula.
" Bado sijajua jinsi ya kuendelea na maisha bila wewe, mwanamume ambaye alinifanya kuwa mama nyaguthii mwanamume ambaye alikuwa na uigizaji moyoni mwakeMwanamume ambaye aliwachukulia waigizaji wenzake kama familia yake, ni pigo kubwa, lala salama Papa." Ilisoma Posti ya Mama Nyaguthii.
Mashabiki wake walimtia moyo na hizi hapa jumbe zao;
phylis_labans MUNGU akwonekanie maama
philipetale It is well
lizmass92 Pole Sana may GOD be with u
mumbe_risper It is well mamii, hugs❤️❤️❤️
