Karne hii ya sasa si kama wakati wa akina babu zetu ambapo walitambua uhusiano wa kimapenzi na hata kuthamini wenzao.
Kuna wale huingia katika uhusiano ili kutimiza hitaji lao la ngono, huku wengine wakitafuta mapenzi ya kweli.
Katika makala haya nitaorodhesha mambo ambapo watu wanapaswa kufahamu kuhusu ngono kabla ya kujihusisha katika uhusiano wowote wa kimapenzi.
1.Ruhusa ni kila kitu
Kama unataka kufanya tendo la ndoa haya basi itisha mpenzi wako ruhusa, kama amesema la, jua ni la na wala husijilazimishe kufanya tendo hilo kama hutaki kuachwa mara moja.
2.Hupaswi kuwa katika uhusiano ili ufanye ngono
Watu wana maono tofauti kuhusu ngono, na ata kuna wale hufuata tamaduni zao kuhusu ngono, kuna wale wanataka tu kufanya tendo la ndoa na kuacha mpenzi wake kwa maana haampendi.
3.Uchumba sio sawa na ngono
Uhusiano wa kimapenzi sio sawa na ngono,kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi uliza mpenzi wako kama yuko tayari kufanya ngono mkiendelea na uhusiano wenu.
4.Wanawake kwanza
Kabla ya kufanya jambo lolote muweke mwanamke wako kwanza kuhusu ngono, na kuzingatia uamuzi wake.