logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Je wanaume ambao hutoa maoni mabaya kuhusu wanawake ni wanyanyasaji?

Kuna baadhi ambao walisema kwamba wanaume ambao hutoa maoni mabaya kuhusu wanawake ni wanyanyasaji.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku04 April 2021 - 08:04

Muhtasari


  • Je wanaume ambao hutoa maoni mabaya kuhusu wanawake ni wanyanyasaji, wa wanawake
sad woman

Kufutwa kwa watangazaji wa homeboyz radio wiki jana, kulijiri saa chache baada ya kutoa maoni mabaya kuhusu mwanamke huku maoni yao yakizua mjadala mkali mitandaoni.

Majadiliano ya watatu hao yalionekana kupendekeza kwamba mwanamke aliyesukumwa nje dirisha la ghorofa ya 12 baada ya kukataa ngono na mpenzi wake anapaswa kulaumiwa kwa kitendo hicho.

Baada ya video ya onyesho kuwekwa mtandaoni, watatu hao walisitishwa na kufutwa kazi, Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki ilivuta matangazo yao kutoka kwa kipindi hicho.

 

Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya iliingilia kati kutoza faini ya milioni 1 kwa homeboyz radio(ambayo inamilikiwa na Radio Africa Ltd) na kusitisha programu hiyo kwa miezi sita.

Hii si mara ya kwanza kwa vyombo vya habari vya Kenya kupeperusha mambo ya dharau juu ya wanawake.

Lakini swali kuu ambalo wengi tumasahau ni kwamba mwanamume anapoamua kumtupa mwanamke kutoka katia ghorofa ya 12 alikuwa anafikiria nini

Pia hamna haja ya kuuliza kwanini mwanamke huyo alikuwa na mwanamume huyo,swali ni je mwanamume huyo alikuwa na akili timamu?

Wanamitandao wengi walitoa maoni tofauti huku baadhi ya wengine wakiwakashifu watangazaji hao kwa ajili ya maoni yao.

Kuna baadhi ambao walisema kwamba wanaume ambao hutoa maoni mabaya kuhusu wanawake ni wanyanyasaji.

Je maoni yako ni yapi kuhusu wanaume ambao hutoa maoni mabaya kuhusu wanawake?

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved