Msanii wa nyimbo za injili Size 8 atatawazwa kuwa mhubiri JUmapili Desemba 12.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyon alitangaza hafla hiyo na kusema kwamba ni jambo lenye hisia kwake.
Atakuwa mhubiri katika kanisa la JCC Thika.Pia alimshukuru mumewe kwa kumshika mkono katika safari yake.
Nitawekwa wakfu kuwa mhudumu wa neno la Mungu, mtumishi wa Mungu aliye juu Jumapili hii na waaaa hiii ni emotionalðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ Mungu si mtu hata aseme uongo
Anamchagua yeyote na kuwabadilisha ili wamtumikie.... Maisha yangu ni sawa na sinema kutoka kwa ulimwengu wa kidunia hadi kwa mtumishi aliyewekwa rasmi wa Mungu ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ muone Mungu......
Nehema za Mungu ni za kweli.... .. Nilizaliwa mara ya pili 2013 nilianza safari ya muziki wa Injili, miaka mitano baadaye 2018 nilisoma shule ya Biblia na kuhitimu na sasa miaka 8 baadaye 2021 naenda kuwekwa wakfu ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ðŸ˜ muone Mungu...
Na kwa Mungu awe utukufu kwa neema yake tu, nguvu zake na roho yake kupitia kwa mwanawe Yesu Kristo imetokea KWA WAKATI WA MUNGU HUFANYA KILA KITU KIZURI!!!
KWA mume wangu @djmokenya asante kwa kuniruhusu kwenda kumtumikia Mungu na kwa Mchungaji na washauri wangu Pastor Kelvin na Jacky Ephraim Mungu awabariki nyote.....