logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mimi sio mjinga, siwezi omba Mbogi genje msamaha - KRG

Msanii KRG amesema kamwe hawezi kuwaomba MBogigenje msamaha.

image
na

Habari11 March 2022 - 05:01

Muhtasari


• Msanii KRG the Don amesema kwamba kamwe hataomba msamaha kwa wasanii wa kundi la Mbogigenje.

• “Mimi ni wazimu? Siwezi omba hao watu msamaha, sina huo muda,” KRG alisema.

Msanii KRG the Don amesema kwamba kamwe hataomba msamaha kwa wasanii wa kundi la Mbogigenje.

Akizungumza katika mahojiano na mwanablogu Nicholas Kioko, KRG alisema kwamba hawezi kujishushia heshima kwa kufanya mazungumzo ya kutafuta amani na wasanii hao.

The Don anasema kwamba alikuwa anatoa msaada kwa Mbogi genje ili muziki wao uende mbali ila wakaamua kuzua vurugu ambayo kamwe hatoikumbatia.

Aliongeza kwamba hana chochote cha kupoteza kwa kutozungumza na wasanii hao, na kuwa yeye ni jamaa ambaye ashatasua katika maisha na kuafikia ndoto zake.

“Mimi ni wazimu? Siwezi omba hao watu msamaha, sina huo muda,” KRG alisema.

Ikumbukwe kwamba kumekuwa na kutupiana cheche baina ya pande hizo mbili huku kila mmoja akivuta kamba upande wake.

Kwa sasa mashabiki wanasubiri kuona iwapo Mbogi genje watakubali kuomba msamaha na angalau kutengeneza mazingira ya amani ambayo pengine yataruhusu ushirikiano wa kazi nyingine katika siku zijazo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved