logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Masomo yatatizwa walimu wakuu 2 wakipigana shuleni, mmoja alikataa uhamisho

Wazazi walihisi kuhamishwa kwa mwalimu wa kwanza ni kutokana na matokeo duni.

image
na Radio Jambo

Habari16 February 2023 - 13:18

Muhtasari


• Hali ilikuwa tete kupelekea mamlaka kuingilia kati na kuitisha mkutano wa kutatua mkanganyiko huo.

Shule moja ya serikali nchini Uganda ilishuhudia kioja baada ya shule kufunguliwa na mwalimu mkuu wa awali kufika na kumkuta mwalimu mkuu mwingine aliyetumwa hapo kuchukua nafasi yake.

Shule hiyo ya Kabaale iliyoko wilaya ya Namutumba ilikumbwa na msukosuko baada ya mwalimu mkuu wa awali kukataa uhamisho na hivyo kulazimika kuwa na walimu wakuu wawili – kila mmoja akidai ndiye mwalimu mkuu wa shule hiyo ya serikali.

Bwana Fred Kagoye Samanya, mwalimu mkuu huyu wa awali, alikataa uhamisho wa kwenda Shule ya Sekondari ya Nakalama wilayani Iganga. Kwa upande mwingine, Bw Stephen Mutono, mwalimu mkuu mpya aliripoti kazini mnamo Februari 6, kulingana na vyanzo kutoka shuleni, jarida la Uganda liliripoti.

Jarida hilo iliripoti kuwa chanzo cha Samanya kuhamishwa hakijulikani ila wanakijiji walihisi ni kutokana na msururu wa matokeo duni katika mitihani ya kitaifa.

Hali hyoi ilisababisha mamlaka zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, na uongozi wa polisi kuitisha mkutano na kutatua mkanganyiko huo.

Mkutano huo ulilenga kusuluhisha mivutano kati ya wazazi na baadhi ya wafanyikazi ambao wametishia kuweka vifaa chini ikiwa Bw Samanya hataondoka shuleni.

Baadhi walisema kwamba mwalimu mkuu wa kwanza hataki uhamisho kwa sababu anaacha shamba kubwa la mifugo aliloanzisha.

 

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved