logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alai: Odinga si kama Amber Ray kuacha Rapudo na kurudi kwa Jimal

Alai alisisitiza kwamba Odinga anataka gharama ya maisha kupungua.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri05 April 2023 - 04:36

Muhtasari


• “Baba havutiwi na chochote zaidi ya gharama ya chini ya maisha kwa Wakenya," - Alai alisema.

Alai asuta makampuni ya kamari kupeleka wachekeshaji Qatar

MCA wa Kileleshwa Robert Alai amefutilia mbali madai kwamba kinara wa Azimio Raila Odinga anataka maridhiano ya kisiasa na Rais William Ruto.

Alai amedokeza haya akiibua mfanano wa mapenzi kati ya mwanasosholaiti Amber Ray na wapenzi wake wa awali Kennedy Rapudo na Jimal Rohosafi.

Alai alisema kwamba Odinga si kama Amber Ray anayeruka kutoka kambi moja kwenda nyingine, akimtaja Ruto kama Jimal na Rapudo kama maandamano.

“Jamani, Baba Raila Odinga si Amber Ray kwa ping-pong kutoka Maandamano (Kennedy Rapudo) hadi kupeana mkono kwa Ruto (Jimal),” Alai alisema.

Baada ya wiki kadhaa za maandamano na kurushiana maneno yasiyopendeza kati ya wanasiasa hao wakuu, Rais Ruto na Bw Odinga walionekana kukaribiana wikendi baada ya kutangazwa kwa mazungumzo ya pande mbili kati ya wawakilishi wa wawili hao.

Mazungumzo hayo yanalenga, miongoni mwa mengine, kusaidia katika kupunguza gharama ya maisha na kushughulikia mageuzi ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wanachama wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

Lakini kumekuwa na ripoti kwamba mazungumzo hayo yanaweza kusababisha Bw Odinga, ambaye alishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Ruto katika uchaguzi wa Agosti 2022 kulingana na data rasmi ya IEBC, kupata sehemu ya serikali.

Lakini kwenye tweet, Alai, ambaye alikuwepo Bw Odinga alipolihutubia taifa na kuthibitisha nia yake ya kushiriki mazungumzo.

Alisisitiza kwamba nia ya Odinga si kutaka handshake bali ni kupigania wakaenya wa kawaida ili gharama ya maisha irudi chini.

Alisema kwamab mambo ya Handshake hayapo kabisa katika kichwa cha Odinga na kuwataka wale wanaotaka hilo kufanay hivyo kwa naibu rais Rigathi Gachagua.

“Baba havutiwi na chochote zaidi ya gharama ya chini ya maisha kwa Wakenya na mchakato bora wa uchaguzi ambao unaimarisha demokrasia yetu. Ni Hayo tu. Handshake mpatieni Gachagua,” Alai alisema.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved