logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pritty Vishy amuomba Stevo Simple Boy warudiane

Pritty Vishy amemuomba Stevo Simple Boy kurudiana baada ya mahusiano yao kutamatika mwaka mmoja uliopita.

image
na

Grafiki31 July 2023 - 07:40

Muhtasari


• Pritty Vishy ameonekana katika live ya TikTok akimuomba Stevo Simple Boy kama wawili hao wangeweza kurudiana.

• Stevo Simple Boy hata hivyo alilikataa ombi la Vishy akidai kuwa hakuwa sawa kiakili kuchumbiana naye lakini angelifikiria ombi hilo na kumpigia ndani ya muda wa miezi mitatu.

Pritty Vishy sasa anataka kurejea katika mahusiano na Stevo Simple Boy

Wikendi, mtayarishaji wa  maudhui Pritty Vishy alimpigia simu na kumuomba aliyekuwa mpenzi wake , Stevo Simple Boy kurudiana naye baada ya mahusiano yao kutamatika mwaka mmoja uliopita.

TikToker huyo kwa muda mrefu baada ya kutengana na Stevo amekuwa akimkashifu hadharani kwa kile alichosema mwanamuziki huyo alikuwa mnyonge sana na hakuweza kujisimamia katika muziki.

Pritty Vishy alionekana katika live ya TikTok japo kwa mzaha akimpigia simu na kumuuliza kama ingekuwa sawa wawili hao wakirudi kwenye mahusiano ombi ambalo Stevo alilikataa mara moja.

“Ngoja akili yangu itulie kwanza, si umeona vile maneno mingi imekuwa kwa mitandao nataka kwanza nitulie na pia nikue sawa kiakili ndio nitakuambia.” Simple Boy alimwelezea Vishy.

Stevo aliongeza kuwa alitumai baada ya miezi tatu angekuwa sawa kiakili na angeweza kufikiria kama itakuwa sawa kurudiana naye.

Mwishoni mwa mwezi Mei, Vishy kupitia akaunti yake ya Instagram alitangaza kuwa hatimaye ameondoka sokoni na kuchapicha picha za mpenzi wake mpya, Dj Starvy huku akionyesha alikuwa tayari kwani kidonda cha kutamatika kwa mapenzi yake na Stevo kilikuwa kishapona.

"Ninapenda kila kitu kuhusu wewe. Unafanya kila kitu kizuri. Unajua unanifanya kichaa, sawa? Nakupenda babe @dj_starvy," alisema.

Starvy alijibu kwa kumhakikishia kipusa huyo mwenye umri wa miaka 21 kuhusu mapenzi yake makubwa kwake.

"Unajua nakupenda mama watoto," alisema.

Mnamo Januari mwaka wa 2022, Pritty alitangaza kuwa mahusiano yake na Simple Boy yalikuwa yametamatika kwa kile alichosema kilikuwa ni kwamba msanii huyo hakuwa akimtetea dhidi ya usimamizi na familia yake.

Vishy Aliibua wasiwasi kwamba msanii huyo anayekua kwa kasi husikiliza kile ambacho usimamizi wake husema bila kuhoji, hata ikiwa ni kinyume na anachoamini.

"Chukulia siku moja Mungu akitubariki tukaoana itakuwaje kwangu, wakwe zangu siku moja watanitembelea na kumtaka anifukuze atafanya hivyo bila pingamizi,” alilalama.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved