logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Flacao ama Falcao? Shabiki apokea jezi isiyo na maandishi sahihi

Flacao ama Falcao? Shabiki apokea jezi isiyo na maandishi sahihi

image
na

Habari02 October 2020 - 17:21
Radamel Falcao tayari amekuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa Manchester United kufuatia uhamisho wake kwa mkopo kutoka Monaco. Wafuasi wengi wa timu hiyo wamekuwa wakinunua jezi na kuandika jina na nambari ya raia huyo wa Colombia mgongoni.

Hivi majuzi shabiki mmoja wa Manchester United alishangaa alipofungua kifurushi aliyotumiwa na duka rasmi ya Manchester United na kupata kuwa jina ya mchezaji ampendaye imeandikwa vibaya. Badala ya "FALCAO", maanadishi yalisoma "FLACAO".

Picha ya jezi ikiwa na maandishi hayo imesambaa sana katika mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook na klabu hiyo inayoshikilia nambari ya 14 katika jedwali ya ligi kuu ya Uingereza imepokea ujumbe nyingi sana ya kuwatania kwa sababu ya kosa hilo.

Kulingana na ujumbe kutoka tovuti ya duka rasmi ya Manchested United, jezi la mkono mifupi ya mtu mkubwa inagharimu pauni 88 (Ksh 12, 572). Ikiwa shabiki atahitaji kuweka maandishi mgongoni bei hiyo itapanda mpaka pauni 105.92 (Ksh 15, 132). Ikiwa shabiki pia atataka kupamba jezi lake na beji ya Premier League, basi itabidi amerudi mfukoni tena na kutoa pauni 6.72 (Ksh 960). Kwa hivyo mtu anaweza tumia kati ya shillingi 12, 572 na 16,100 kununua jezi moja ya Manchester United kutoka kwa duka lake rasmi. Baada ya kutumia fedha hiyo yote itakuwa jambo la kughadhabisha sana kupata kuwa maandishi katika jezi si sahihi na lazima shabiki huyo alihisi vivyo hivyo.

Si mara kwanza Manchester United wamefanya kosa kama hilo. Wachezaji wa timu hiyo kama Anderson, David Beckham, Tomasz Kuszczak na Ole Gunnar Solksjaer wamewahi vaa jezi yenye maandishi yasiyo sahihi.

Makosa ya maandashi kama hayo huonekana sana na watu ambao wana tatizo ya kusoma ijulikanyo kama "dyslexia". Watu ambao wameathirika na tatizo hilo hushindwa kutabiri vizuri wanachosoma na kuandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved