logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kijana ajitia kitanzi baada ya mamake kupuuza mwito wake

Kijana ajitia kitanzi baada ya mamake kupuuza mwito wake

image
na

Habari02 October 2020 - 16:16

Picha kwa hisani ya: elcrema.com

Kijana mmoja kwa jina Antony Otieno mwenye umri wa miaka 20 kutoka katika kijiji cha Nyawara amejitoa uhai kwa madai ya kuachwa na mamake aliyeelekea Nairobi kazini.

Inadaiwa kuwa kijana huyo alimtaka mamake kujenga kabla ya kurejea Nairobi anakotafuta riziki lakini mamake alipuuza agizo la mwanawe na kuwaacha na nyanyao swala lililo mkasirisha marehemu na kuamua kujitia kitanzi.

Kulingana na baadhi ya wanafamilia kijana huyo alionekana mwingi wa mawazo hapo jana na pindi alipomaliza kula chakula cha jioni alitoweka nyumbani kabla ya mwili wake kupatikana ukininginia leo asubuhi kwenye mti wa maembe.

Akithibitisha kisa hicho chifu wa eneo hilo David Otieno amewataka wazazi kuwapa ushauri wanao hasa wanapoonekana kusongwa na mawazo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved