picha: the-star.co.ke
Wenyeji wa mtaa wa Elgon, katika barabara ya Kisumu-Kibos walishuhudia kisa ambacho si cha kawaida wakati jamaa mmoja anayedaiwa kuwa mwizi wa pikipiki kujitokeza na kurejesha pikipiki aliyokua ameiba huku akiwa uchi wa mnyama.
Inadaiwa kuwa jamaa huyo alilazimika kufanya hivyo baada ya kuzidiwa na nguvu za mganga aliyeitwa kumtafuta mwizi wa pikipiki hiyo.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, pikipiki hiyo iliibwa kutoka eneo la Obunga baada ya siku kadhaa bila kuona pikipiki yake, mwenyewe aliamua kutafuta usaidizi kutoka kwa mganga.