Ufasaha wake katika lugha ya taifa na ubabe wake ni mojawapo tu ya sifa ambazo zimejaa kwenye hazina lake, ambalo limemfanya kuwa nyota linalong'aa katika wingu la sanaa ya uanahabari kila uchao.
Yusuf Juma anayetambulika kwa jina la utani kama 'YJ', anatambulika zaidi miongoni mwa mashabiki wa Radio Jambo kwa sauti ya kina, huku wengi wao wakiisifia kama sauti iliyo na uwezo wa kutoa nyoka pangoni. Licha ya kusoma habari kila baada ya saa na nusu saa kila siku ya wiki, kutoka mida ya saa kumina mbili hadi saa nne, mwanahabari huyu wa miraba minne pia ana kitengo cha 'Kiswahili sio mdomo wetu'.
Also read:
Kupitia kitengo hiki, zaidi ya wakenya millioni 10 hupata fursa ya kujifunza maneno au majina mapya ya Swahili.
Lakini je, ni yepi haswa huendelea wakti wa usomaji habari?.
Kupitia mtandao wake wa Youtube bwana YJ alijibu swali hilo baada ya kuchapisha kanda yake, huku akionesha ubabe wake nyuma ya kipaza sauti,.
Tazama mwanahabri huyu akisoma habari moja kwa moja kutoka studio za Radio Jambo.
&feature=youtu.be