Naam kama alivyokiri mwenyewe alisema kuwa kando na kuwa mwanabiashara aliyesifika, ni mpenzi wa kusakata densi huku akipuuzilia mbali kuwa ana talanta katika nyanja hiyo.
"Napenda kucheza ngoma sana." Alisema Massawe huku akiangua kicheko. "Siwezi sema kuwa nina talanta au nina ubora katika usakataji densi lakini najua jinsi ya kusakata densi." Aliongeza huku akisema kuwa jambo linalompa furaha zaidi ni kutumia wakati wake mwingi pamoja na familia yake.
Huku tukiunganisha hayo mawili, inadhihirika wazi katika kanda ambayo imechapishwa kuwa kusakata densi ndio njia moja kuu inayoileta pamoja familia yake mtangazaji huyu wa kipindi cha Bustani la Massawe ambacho huja kwako kila siku ya wiki kuanzia mida ya saa nne hadi saa nane.
Japanni alirekodi kitengo maalum huku yeye na wanawe wakijivinjari kwa kusakata densi na mdundo wa kisasa ambao vijana waufahamu kuliko yeyote yule.
Kando na kucheza mdundo wa kisasa, aliwashangaza wengi huku akisakata pia kwa mitindo ya kisasa huku akionyesha umaahiri wake.
Tazama kanda ifuatayo.
&feature=youtu.be