logo

NOW ON AIR

Listen in Live

MIGORI: Polisi Wanasa Bangi Ya Milioni Moja

MIGORI: Polisi Wanasa Bangi Ya Milioni Moja

image
na

Habari01 October 2020 - 16:15
bangi
Polisi wakishirikiana na umma wameteketeza bangi ya milioni moja nukta mbili iliyotolewa katika shamba moja la nusu ekari kwenye eneo la Suna kwenye kaunti ya Migori.

Kulingana na kamishna wa polisi wa kaunti ya Migori, Seif Idd Matata na kamanda wa polisi wa Migori David Kirui polisi walipata habari kuhusu bangi hiyo kutoka kwa umma na kuelekea katika shamba hilo la ekari tatu kuanza kuing’oa.

Maafisa hao wakuu wa usalama wa kaunti ya Migori waliamrisha maafisa hao kutoa ulinzi kwa bangi hiyo na kutaka bangi hiyo kupelekwa katika afisi za kamishna wa kaunti ya Migori ambako iliteketezwa kwa kuchomwa na mafuta ya petrol.

Polisi wamedai kuwa kaunti ya Migori imekumbwa na visa vingi vya bangi kunaswa katika maeneo tofauti na kuchangia katika ukosefu wa usalama mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Wameapa kumaliza visa vya ulanguzi wa madawa ya kulevya ikiwemo bangi  na aina tofauti ya mihadarati.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved